Arsène Wenger:Hakuna mazungumzo na
Barcelona kuhusu Song.
Meneja wa Arsenal
Arsene Wenger amesisitiza kuwa kuwa mpaka sasa hakuna maombi yoyote klabu
yoyote ikiwemo Barcelona juu ya kiungo wake Alex Song.
Kiungo huyo
wa kimataifa wa Cameroon amekuwa akiarifiwa kutakiwa na bosi mpya wa Barcelona
‘Blaugrana’ Tito Vilanova, lakini Wenger ametupilia mbali fununu hizo katika
kujenga vizuri hatma ya kikosi chake.
Bosi huyo
mfaransa amesisitiza kuwa hakuna mawasiliano yaliyofanywa baina ya pande hizo
mbili na amekanusha taarifa hizo ambazo zimetapakaa katika vyombo vya habari
nchini Hispania.
"hakuna
kinachoendelea kuhusu Song,"
"Song ana
mkataba wa miaka mitatu tofauti na hali ilivyo kwa Robin van Persie.
Wakali watajwa kwenye orodha ya UEFA.
Andres Iniesta, Lionel Messi na Cristiano
Ronaldo wametajwa katika orodha fupi ya wachezaji bora wa shirikisho la soka
barani ulaya UEFA.
Wachezaji
watatu miongoni mwao walikomba points nyingi katika mzunguko wa kwanza wa
kupigiwa kura kwa ajili ya tuzo hiyo ambayo itatolewa mjini Monaco August 30.
Wachezaji
pacha wa Barcelona Iniesta na Messi wanajiunga na nyota wa Real Madrid Ronaldo
wakati ambapo kiungo wa Juventus Andrea
Pirlo na Xavi Hernandez wakikosekana katika orodha.
Orodha ya mwisho
imetolewa na mwandishi mmoja wa habari kutoka nchi wanachama wa UEFA ambao
wanawapigia kura wachezaji watano.
Kakuta anasaka mlango wa kutokea Chelsea
Gael Kakuta |
Gael Kakuta amesema
anafikiria kuondoaka Chelsea kusaka timu atakayo pata nafasi ya kucheza katika
kikosi cha kwanza na sasa na ana mpango wa kuelekea Marseille.
Mfaransa
huyo anayechezea timu ya vijana ya Ufaransa huko nyuma alikuwa katika nafasi
nzuri ya kucheza kikosi cha kwanza wakati huo akiitumikia kwa mkopo katika
vilabu vya Fulham, Bolton na Dijon.
Kwasasa
anasaka fursa nje ya Chelsea kuliko kuendelea kusalia katika kikosi hicho
ambacho yuko kwenye mkataba wa miaka mitatu.
Akiongea na L'Equipe
amesema
"mkurugenzi wa michezo wa Chelsea Michael
Emenalo alianimbia mwezi July kuwa itategemea na maamuzi ya kocha. nasubiri
kuona nini kitatokea”.
Manchester City iko katika mpango wa kumuajiri
makamu wa Rais wa zamani wa Barcelona vice-president Soriano kuwa mtendaji mkuu
Ferrano Soriano |
Manchester
City iko katika mpango wa kumuajiri makamu wa Rais wa zamani wa Barcelona Ferran
Soriano kuwa mtendaji mkuu wa klabu hiyo kufuatia mapinduzi makubwa ndani ya
klabu hiyo akichukua nafasi ya Garry Cook.
Mabingwa hao
wa Premier League wako katika mwelekeo mwingine wa kumnasa mtendaji huyo baada
ya kuvunjika kwa Spanair, shirika la ndege ambalo lilikuwa likiongozwa na
mtendaji huyo wa zamani wa Barca.
Katika hatua
nyingine City imekuwa katika mazungumzo na Soriano ambayo yameanza upya masaa
24 yaliyopita ambayo huenda yamepelekea mabadiliko hayo ya kujaza nafasi hiyo
muhimu.
Taarifa toka
kwa watu wa karibu na mabigwa hao wa ligi kuu ya Uingereza wamesema Soriano anakaribia
kuchukua nafasi ya kazi na akiajiriwa kama CEO na huenda akatangazwa rasmi
ndani ya siku saba kuanzia sasa.
No comments:
Post a Comment