Washiriki kutoka Nigeria |
Prof. Ludwig Guttmann |
Ulikua mwaka 1948, hospitali iliyo nje kidogo
ya mji mkuu wa London ilishuhudia mwanzo wa vuguvugu la mashindano ya walemavu,
baada ya daktari aliyekimbia utawala wa Nazi nchini Ujeremani mwenye asili ya
Kiyahudi kujaribu kubadili maisha ya wagonjwa walioathiriwa na majeraha ya uti
wa mgongo -- na hivyo kuwatia moyo washiriki michezo.
Michezo ya
kwanza iliyojulikana kama "Stoke Mandeville Games" ilipangwa mwaka
1948 ili ifanyike sambamba na mashindano ya mwaka huo yaliyofanyika nchini
Uingereza.
Jina
Mandeville ni la Hospitali ya huko Buckinghamshire ambako Prof. Ludwig Guttmann
aliongoza juhudi zake za tiba ya kiakili kwa wagonjwa wa uti wa mgongo
walioshiriki michezo ya mwaka huo, wakiwa wanaume 14 na wanawake 2 walioshiriki
wakiwa ndani ya magari ya walemavu na kushiriki mashindano ya kulenga mishale.
Wengi wao
walikua ni wanajeshi waliojeruhiwa katika vita vikuu vya pili vya Dunia.
Mwaka mmoja
baadaye timu sita zilishiriki michezo huko Stoke Mandeville -- kukiwa na
mashindano ya netiboli, mchezo uliotangulia mchezo wa kikapu -- wakati michezo
ikitumiwa kama sehemu ya matibabu ya wagonjwa kama ilivyopengekezwa na
Guttmann.
Mwaka 1956,
''taarifa ya dhamira''ilizinduliwa kwa ajili ya Michezo hii ambayo wakati huu
ilikuwa ni ya Kimataifa kwa mujibu wa wavuti ya kumbukumbu za Mandeville
inayodhaminiwa na mamlaka ya wilaya hiyo.
Taarifa hiyo
ilisema 'dhamira ya michezo ya Stoke Mandeville ni kuwaunganisha wanaume kwa
wanawake waliopooza viungo kutoka sehemu zote za Dunia katika vuguvugu hili la
michezo ya Kimataifa, pamoja na moyo wa wanamichezo hii leo kuwapa matumaini na
kuwa kivutio kwa maelfu ya walemavu.
Miaka minne
baada ya hapo, wakivutiwa na muongozo wa Guttman, mashindano ya kwanza ya
Walemavu yakafanyika mjini Roma sambamba na Olimpiki.
Miaka
hamsini baada ya michezo ya kwanza kwa walemavu, washiriki 4,280 kutoka mataifa
165 -- ikiwa ni idadi kubwa kuwahi kujitokeza kushiriki -- wamerejea Uingereza
kushiriki mashindano ambayo hivi sasa yanashirikisha watu waliozaliwa na hali
hio kutokana na sababu mbalimbali labda ajali au kusababishwa na maradhi.
Tangu
michezo hii ianzishwe huko Stoke Mandeville, mahali ambapo jina lake limetumiwa
katika nembo na mleta bahati mwenye jicho moja au ''Mascot'' ya michezo hii
Michezo hii imepiga hatua kubwa.
Lengo la
mashindano haya siyo kuwapima uwezo, bali kuwawezesha kufurahia uwezo wao moyo
wa iuchezo hii umebaki pale pale.
No comments:
Post a Comment