Kiungo wa Liverpool
Lucas Leiva atakuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi mitatu ya msimu baada ya
kupata majeraha katika paja lake yaliyotokana na mazoezi wakati wakijiandaa kwa
ajili ya mchezo dhidi ya Manchester City.
Lucas Leiva atakosekana
kwa miaezi mitatu hii ni kwa mujibu wa meneja wake manager Brendan Rodgers. Mbrazil
huyo kiungo wa chini hakumudu kuendelea na mchezo baada ya dakika katika mchezo
dhidi ya Manchester City uliopigwa jumapili.
Lucas amepata
maumivu hayo wakiwa katika muda wa kupasha misuli moto kabla ya kuivaa Manchester
City, lakini hata hivyo alianzishwa katika mchezo huo licha ya maumivu
aliyoyapata na kuishia kunako dakika ya nne ya mchezo ambapo alibadilishwa na
kuingizwa Jonjo Shelvey.
Hilo ni pigo
kubwa kwa Lucas, ambaye hivi karibuni amerejea kutoka katika maumivu mengine ya
msuli ambayo yalimuweka nje ya uwanja katika sehemu kubwa ya msimu uliopita.
Hata Rodgers
anaamini kuwa Lucas anaweza kuponya haraka majeraha yake na kuongeza kuwa ni
mchezaji ambaye huwa anaponya majeraha yake haraka hivyo anamtegemea kuwa naye
mapema zaidi ya hapo
Lucas atakosa
michezo kadhaa ukiwemo mchezo dhidi ya Manchester United maarufu kama ‘Merseyside
derby’. Kupitia mtandao wa Twitter Lukas ameonyesha kusikitishwa kwake na
majeraha mengi aliyoyapata.
“sina la
kusema kwasasa kwa jinsi ninafikiria , ni ngumu kuelezea kwa sasa siko sawasawa
lakini naamini siku njema zitawadia siku moja”

No comments:
Post a Comment