Timu ya Taifa
ya Tanzania chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) sasa itaivaa Misri kwenye raundi
ya pili ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za 10 za Afrika kwa
vijana chini ya miaka 17 zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Awali
Serengeti Boys ilikuwa icheze raundi ya kwanza dhidi ya Kenya, mechi ya kwanza
ikichezwa Septemba 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Shirikisho la
Mpira wa Miguu la Kenya (FKF) jana lilituma taarifa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF) likielezea kujitoa kwenye michuano hiyo.
Serengeti
Boys itaanzia nyumbani Oktoba 14 mwaka huu, wakati ya marudiano itachezwa nchini
Misri kati ya Oktoba 26-28 mwaka huu. Mshindi baada ya mechi hizo mbili ataingia
raundi ya tatu ambayo ndiyo ya mwisho kabla ya kwenda Morocco.
Katika raundi
ya tatu ambayo mechi zake zitachezwa katikati ya Novemba na ya marudiano mwisho
mwa mwezi huo, mshindi kati ya Tanzania/Misri atacheza na mshindi wa mechi ya
Congo Brazzaville dhidi ya Msumbiji/Zimbabwe ambazo zinapambana katika raundi ya
kwanza.
Wachezaji
wanaounda kikosi cha Serengeti Boys chini ya Kocha Jakob Michelsen ni makipa
Abdallah Bakar (Mjini Magharibi), Hamad Juma (Azam) na Peter Manyika (JKT Ruvu).
Mabeki ni
Abdallah Salum (Mjini Magharibi), Basil Seif (Morogoro), Hassan Mganga
(Morogoro), Ismail Gambo (Azam), Mgaya Abdul (Azam), Miraji Selemani (Polisi
Morogoro), Miza Abdallah (Kinondoni), Mohamed Hussein (Azam), Pascal Matagi
(Dodoma) na Paul James (Kinondoni).
Viungo ni
Farid Musa (Kilimanjaro), Hussein Twaha (Coastal Union), James Mganda (Kipingu
Academy), Mbwana Ilyasa (Simba), Mohamed Haroub (Zanzibar), Mohamed Kapeta
(Kinondoni), Mudathiri Yahya (Azam), Mzamiru Said (Morogoro) na Selemani Bofu
(JKT Ruvu).
Washambuliaji
ni Abdallah Kisimba (Mwanza), Calvin Manyika (Rukwa), Dickson Ambunda (Mwanza),
Joseph Lubasha (Azam), Kelvin Friday (Azam) na Salvatory Nkulula (Kipindu
Academy).
MCHEZAJI
AOMBEWA ITC UJERUMANI
Chama cha
Mpira wa Miguu cha Ujerumani (DFB) kimetuma maombi ya kupatiwa Hati ya Uhamisho
wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya mchezaji Robert Makanja ili aweze kucheza mpira
wa miguu nchini humo.
DFB imetuma
maombi hayo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ili kumwezesha mchezaji
huyo kuichezea timu ya TUS Ahausen, Hessischer FuBall-Verband ambayo hata hivyo
haikuelezwa iko ligi ya daraja gani nchini humo.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mashindano wa DFB, Markus
Stenger, Mtanzania huyo ameombewa hati hiyo kama mchezaji wa ridhaa kwa maelezo
kuwa hakuwahi kusajiliwa na klabu yoyote nchini.
TFF inafanyia
kazi maombi hayo na hati hiyo itatolewa mara baada ya taratibu husika kukamilika
ikiwemo kubaini kama kweli mchezaji huyo hakuwahi kusajili na klabu yoyote hapa
nchini.
Boniface
Wambura Mgoyo
Ofisa
Habari
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment