Coentrao nje michezo minne, kukosa pia Supercopa Clasico
Kocha wa Real
Madrid Jose Mourinho atalazimika hii leo kukosa huduma ya mlinzi wake wa
kushoto Fabio Coentrao kufuatia shirikisho la soka nchini Hispania kumfungia
mlinzi huyo kwa michezo minne kutokana na kupewa kadi nyekundu katika mchezo
ambao Madrid walifungwa na Getafe mabao 2-1 mchezo uliopigwa jumapili iliyopita.
Coentrao
alimwita mwamuzi Miguel Angel Perez Lasa mtoto wa malaya katika mchezo huo na kamati ya nidhamu imeamua
kumfungia kucheza kwa michezo minne .
Mlinzi huyo
mwenye umri wa miaka 24 atakosa michezo ya ligi ya Hispania La Liga dhidi ya Granada,
Sevilla, Rayo Vallecano pia mchezo wa marudiano wa Spanish Supercopa hii leo.
Aidha kocha
wa Barcelona Tito Vilanova amesimamishwa kuketi katika benchi la ufundi kwa
michezo miwili kufuatia kwenda kinyume na nidhamu ya benchi inavyotaka katika
mchezo dhidi ya Osasuna uliopigwa jumapili.
Vilanova mwenye
umri wa miaka 42 alionekana mara kadhaa katika mchezo huo akilalama kwa hasira juu
ya maamuzi ya mwamuzi wakati mchezo ukiendelea licha ya kuonywa na mwamuzi
msaidizi, ambapo aliondoshwa katika benchi na mwamuzi wa mchezo kunako dakika
ya 70 ya mchezo huo.
Hata hivyo
msaidizi huyo wa zamani wa Pep Guardiola atakosekana katika michezo dhidi ya Valencia
na Getafe kwa kuwa kosa lake si kubwa kama ilivyo kwa Coentrao.
Rais wa Inter
Milan, Massimo Moratti ameweka wazi kuwa haoni sababu ya kwanini Maicon aihame
klabu yake msimu huu wa uhamisho wa kiangazi.
Mlinzi huyo
wa kulia wa kimataifa wa Brazil, bado ameendelea kuhusishwa na kutaka kuondoka Nerazzurri,
na wakala wake akinukuliwa wiki iliyopita akisema kuwa vilabu kama Chelsea,
Manchester City na Real Madrid vimekuwa vikionyesha nia ya kumsaini mlinzi huyo
wa kulia.
Aidha wakati
msimu wa uhamisho ukikaribia kufungwa huku Maicon akiachwa katika orodha ya
wachezaji wa Inter kwenye kikosi kitakacho cheza dhidi ya Pescara ukiwa ni
mchezo wa ufunguzi wa msimu wa Serie A, inaonekana wazi kuwa atasalia.
Alipoulizwa
Morati na La Gazzetta Dello Sport juu ya Maicon na hatma yake ya baadaye
alijibu "Maicon? Hebu tusubiri tuone nini kitatokea . Anaweza kusalia hapa
na kufanya vizuri”.
"Nilimpenda
alifanya vizuri katika mchezo dhidi ya Pescara. Ameonyesha kuwa yuko katika hari ya
juu kimchezo na anatumia akili. Tumtumainiye kuwa ataendeleza hilo"
Inter kesho
itakuwa ikicheza mchezo muhimu wa marudiano ukiwa ni mchezo wa Europa League ‘playoff’
dhidi ya dhidi ya Vaslui.
No comments:
Post a Comment