Terry na Gerrard warudishwa timu ya
taifa ya England
Meneja wa
timu ya taifa ya England Roy Hodgson amewarejesha katika kikosi cha timu ya
taifa ya John Terry na Steven Gerrard kwa ajili ya michezo miwili ya kuwania
kufuzu fainali ya kombe la dunia dhidi ya Moldova na Ukraine.
Terry kwasasa
anakabiliwa na uchunguzi toka chama cha soka cha England FA kufuatia tuhuma za
kibaguzi msimu uliopita dhidi ya mlinzi wa QPR Anton Ferdinand na aliachwa
katika kikosi kilichocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Itali.
Nahodha huyo
wa Chelsea pamoja na kiungo mzoefu wa Liverpool Gerrard, wamerejeshwa kikosini
lakini mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney na mlinzi Rio Ferdinand wameachwa kufuatia kusumbuliwa
na majeraha.
Walinda mlango
Jack Butland na John Ruddy, ambao waliitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi
kilichocheza dhidi ya Italia wamejumuishwa tena wakiwa pamoja na mlinda mlango
namba moja Joe Hart.
Katika upande
wa ulinzi nyota vijana Ryan Bertrand na Kyle Walker wanaungana na Terry, Ashley
Cole na Joleon Lescott, wakati ambapo katika sehemu ya kiungo Tom Cleverley ameendelea
kusalia katika kikosi hicho baada ya kuonyesha kiwango katika mchezo dhidi ya
Italia pamoja na Michael Carrick.
Ushambuliaji
, Andy Carroll amechaguliwa tena na ataungana na Jermain Defoe, Danny Welbeck na
Daniel Sturridge.
Xavi: Barca ingeweza kuichapa Madrid licha
ya kuwa pungufu.
Xavi anasema
Barcelona ilikuwa na nafasi ya kuichapa Real
Madrid hapo jana licha ya kusalia 10 uwanjani na hilo lingewezekana hata kabla
ya mapumzikoni ambapo Adriano alitolewa
kwa kadi nyekundu.
Catalans katika
mchezo huo walifungwa mabao 2-1 mchezo uliopigwa Santiago Bernabeu, na
kuwafanya Madrid kushinda Spanish Supercopa kwa faida ya magoli mawili ya
ugenini ambapo Barca walifungwa mabao 3-2 kule Nou Camp.
Kama hiyo
haitoshi kiungo huyo mwenye mvuto anapokuwa uwanjani alionyesha soka la kuvutia
katika timu hasa katika kipindi cha pili.
Amenukuliwa akisema
"makosa
mawili na kadi nyekundu yalitugharimu, ukiachana na hilo tulirudi kwenye mchezo
vizuri na pengine tungeshinda Supercopa pamoja na kwamba tulikuwa 10"
"tuliendelea
kucheza mpira wetu kwa style ya uchezaji wetu licha ya upungufu wetu. Kipindi cha
pili tulitengeneza nafasi nyingi ambazo zingetuwezesha kushinda taji."
Hata hivyo
amewataka wachezaji wenzake kusahau Supercup na kurejea La Liga ambapo Barcelona watakuwa
wenyeji wa Valencia jumapili.
Martinez ana kazi kikosi cha kwanza Munich
Licha ya
kutengeneza rekodi ya usajili katika soka la nchini Ujerumani , Javi Martinez anakabiliwa
na vita kubwa ya kupata namba katika timu yake ya Bayern.
Mkurugenzi wa
Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amenukuliwa akisema .
"kama
atakuwepo katika kikosi dhidi ya Stuttgart jumapili hilo ni jukumu la kocha "
Tayari kuna
ushindani mkubwa katika eneo la kiungo katika viunga vya Allianz Arena, huku
pia changamoto kubwa ikiongezwa na Basque.
Moja ya
sababu ya Martinez kukubali kujiunga na Bayern inaelezwa kuwa ni kuhakikishiwa
kutumika kama mchezaji wa kiungo kuliko ulinzi ambayo alikuwa akichezea
alipokuwa na Athletic Bilbao msimu uliopiota jambo ambalo lilikuwa likimkwaza.
Martinez,
alii gharimu Bayern kitita cha euro milioni €40 ambacho atalazimika kupigana
kweli kweli ili kupata nafasi ya kucheza katika nafasi hiyo ambayo ya kiungo
mzuiaji ambapo kuna Bastian Schweinsteiger, Toni Kroos, Luiz Gustavo na Anatoli
Tymoschtschuk ambao nao wanagombea nafasi hiyo.
Lakini Schweinsteiger
ambaye hakuwa ni mwenye bahati kuelekea kumalizika kwa msimu sasa amerejea
vizuri na Martinez atalazimika kujenga 'great
partnership' hiyo ikiwa ni kauli ya nguli katika soka la Ujerumani Franz
Beckenbauer.
Hiyo inaweza
ikawafanya Gustavo, ambaye alisajiliwa kwa euro milioni €17 akitokea Hoffenheim
19 mwezi uliopita pamoja Tymotschtschuk kuwa na makazi ya kudumu katika benchi.
Mshambuliaji
wa Tottenham Hotspur Jermain Defoe ameingia mkataba mwingine na klabu yake hiyo
ambao utamaliza minongono ya kuwa alikuwa katika mipango ya kuondoka White Hart
Lane.
Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa England alikuwa akifikia ukiongoni kwa muda chini ya kocha
wa zamani wa Spurs Harry Redknapp lakini akaahidiwa kipindi kingine na maisha
ndani ya klabu hiyo na Andre Villa-Boas.
Defoe amenukuliwa
kupitia katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter akisema
"ni
wiki nzuri kwa nimesaini mkataba mpya na spurs & na kujumuishwa katika
kikosi cha England kwa ajili ya michezo muhimu #goalsgoalsgoals."
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 29 amejumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya England
na kocha Roy Hodgson kwa ajili ya
michezo miwili ya kuwania kufuzu fainali ya kombe la dunia dhidi ya Moldova na Ukraine.
Defoe mwenyewe
alisikika akisema kuwa katika mashaka juu ya hatma yake ya baadaye na Spurs kiasi
kutangaza kuwa huenda akatafuta njia ya kuelekea endapo hata hakikishiwa nafasi
katika kikosi cha kwanza.
Villas-Boas alikuwa
akihusishwea na kutaka kuwasajili washambuliaji kadhaa wakiwemo Leandro Damiao,
Loic Remy na Willian, lakini inaonekana hilo limezimwa na usajili wa Defoe,
Emmanuel Adebayor na kinda Harry Kane.
Julio cesar
aliyesajiliwa hivi karibuni na Queen's Park Rangers anaamini endapo wachezaji
wenzake watajiamini basi wanaweza kutwaa taji la ligi kuu ya nchini ENGLAND.
Cesar,ambaye
ana umri wa miaka 32, anaamini hakuna kisicho wezekana pale Loftus Road hasa
ikizingatiwa kuwa ni kiasi kikubwa cha pesa kimeahidiwa kutolewa na mmiliki wa
klabu hiyo Tony Fernandes kwa ajili ya kununua wachezaji wapya.
Amenukuliwa na
Daily Mail akisema
"nina
ndoto nyingi sana na QPR, kikubwa ni kucheza vizuri kwa ajili ya mashabiki,
meneja , mwenyekiti na wewe mwenyewe".
Anasema endapo
watafanya hivyo hatimaye watamaliza ligi katika nafasi nne za juu na kufuzu kwa
ajili ya vilabu bingwa ulaya na baadaye siku zijazo kuna uwezekana wa kutwaa Premier
League.
Cesar
ametolea mfano kuwa ziku chache zilizo pita hakuna aliyedhani kuwa Manchester
City ingeweza kutwaa taji la Premier League, Lakini ukiweka nia hilo linaweza
kutokea.
Mlinda mlango
huyo ametoa kauli hiyo baada ya kuona Rangers ikianza vibaya msimu lakini
anadhani mambo yataimarika katika kikosi hicho cha kocha Mark Hughes.
Akiwa katika
kikosi Rangers msimu huu, mlinda mlango huyo wa zamani wa Inter Milan anakabiliwa
na ushindani mkubwa wa kukalia lango la timu hiyo kutoka kwa Rob Green.
No comments:
Post a Comment