Mlinzi wa
kimataifa wa klabu ya Yanga Mbuyu Twite amepata mapokezi makubwa hii leo katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati beki huyo alipowasili
akitokea Rwanda.
Nyimbo za
Mbuyu Mbuyu Mbuyu na kelele nyingine zikimbeza mwenyekiti wa Simba Ismail Aden
Rage zilisikika zikiimbwa na mamia ya
mashabiki wa Yanga wake kwa waume waliofurika uwanjani hapo kwaajili ya
kumpokea beki huyo.
Mara baada
ya kuwasili uwanjani hapo majira ya saaa10.30 jioni,Twite aliyepokewa na viongozi
wa Yanga wakiongozwa na katibu mkuu,Selestine Mwesigwa alikabidhiwa jezi namba
4 yenye jina la Rage kama ishara ya ushindi
dhidi ya wapinzani wao Simba.
Mara baada
ya kukabidhiwa jezo hiyo,Twite alizungumza na waandishi wa habari na kusema
kuwa umati alioushuhudia uwanjani hapo ulimpa moyo wakuona jinsi mashabiki
wanamjali.
Baada ya
mahojiano na Wanahabari, Twite alipanda
gari dogo na moja kwa moja msafara ulioongozwa na mabasi madogo aina ya
Coastal ulielekea makao makuu ya Yanga yaliyoko Mtaa wa Jangwani.
Twite anatarajiwa kuonekana dimbani kwa mara ya kwanza akiwa na jezi ya Yanga jumamosi uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam pale ambapo mabingwa hao wa kombe la Kagame watakapokuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Coast Union ya Tanga ukiwa ni mmoja ya michezo ya maandaliazi ya ligi kuu ya soka Tanzania. Bara.
No comments:
Post a Comment