Wakati kamati ya
Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa
ikitarajia kukutana Jumapili (Septemba 2 mwaka huu) kupitia usajili wa
wachezaji kwa msimu wa 2012/2013, taarifa zinasema kumejitokeza idadi kubwa ya mapingamizi ambao watajadiliwa katika kikao hicho.
Usajili
utakaopitiwa ni wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Lidi Daraja la Kwanza
(FDL) ambapo Kamati itapitia pingamizi zilizowasilishwa na klabu mbalimbali
dhidi ya wachezaji waliosajiliwa na klabu zingine.
Mbali na mapingamizi ya akina Kelvin Yondani Mbuyu Twite na Ramadhani Chombo Lidondo mapingamizi mengine mengi yamejitokeza toka kwa vilabu mbalimbali.
Miongoni mwa vilabu vilivyo weka pingamizi ni pamoja na Kagera Sugar ambayo inapinga David Luhende kwenda
Yanga kwa vile hajafanyiwa uhamisho. Flamingo ya Arusha inapinga wachezaji wake
Kelvin Friday Idd kwenda Azam na Salim Walii kwenda Polisi Mara kwa vile
hawajafanyiwa uhamisho. Toto Africans inapinga wachezaji wake Enyinna Darlinton
kwenda Kagera Sugar na Mohamed Soud kwenda Coastal Union kwa vile bado ina
mikataba nao. Hao ni baadhi tu ya wanaopingwa, lakini wako wengi.
No comments:
Post a Comment