SERENGETI
BOYS, KENYA KUCHEZA AZAM COMPLEX
Mechi ya
kwanza ya raundi ya kwanza kuwania tiketi ya kucheza Fainali za 10 za Afrika
kwa vijana chini ya miaka 17 zitakazofanyika mwakani nchini Morocco kati ya
Tanzania (Serengeti Boys) na Kenya itachezwa Septemba 9 mwaka huu Uwanja wa
Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Tayari
Serengeti Boys chini ya Kocha Jakob Michelsen na Msaidizi wake Jamhuri Kihwelo
ikiwa na wachezaji 28 iko kambini jijini Dar es Salaam tangu jana (Agosti 27
mwaka huu) kujiandaa kwa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni.
Wachezaji
waliko kambini ni makipa Abdallah Bakar (Mjini Magharibi), Hamad Juma (Azam) na
Peter Manyika (JKT Ruvu). Mabeki ni Abdallah Salum (Mjini Magharibi), Basil
Seif (Morogoro), Hassan Mganga (Morogoro), Ismail Gambo (Azam), Mgaya Abdul
(Azam), Miraji Selemani (Polisi Morogoro), Miza Abdallah (Kinondoni), Mohamed
Hussein (Azam), Pascal Matagi (Dodoma) na Paul James (Kinondoni).
Viungo ni
Farid Musa (Kilimanjaro), Hussein Twaha (Coastal Union), James Mganda (Kipingu
Academy), Mbwana Ilyasa (Simba), Mohamed Haroub (Zanzibar), Mohamed Kapeta
(Kinondoni), Mudathiri Yahya (Azam), Mzamiru Said (Morogoro) na Selemani Bofu
(JKT Ruvu).
Washambuliaji
ni Abdallah Kisimba (Mwanza), Calvin Manyika (Rukwa), Dickson Ambunda (Mwanza),
Joseph Lubasha (Azam), Kelvin Friday (Azam) na Salvatory Nkulula (Kipindu
Academy).
Mechi ya
marudiano itachezwa jijini Nairobi, Kenya kati ya Septemba 21, 22 na 23 mwaka
huu. Timu itakayofanikiwa kusonga mbele itacheza raundi ya pili dhidi ya Misri.
Mechi ya kwanza itachezwa nyumbani kati ya Oktoba 12, 13 na 14 mwaka huu wakati
ya marudiano itakuwa kati ya Oktoba 26, 27 na 28 mwaka huu.
Misri ni
kati ya timu 17 zilizoingia moja kwa moja raundi ya pili. Nyingine ni Afrika
Kusini, Algeria, Burkina Faso, Cameroon, Congo Brazzaville, Cote d’Ivoire,
Gabon, Gambia, Ghana, Guinea, Mali, Rwanda, Senegal, Sierra Leone, Tunisia na
Zambia.
KAMATI YA
SHERIA KUPITIA USAJILI SEPT 2
Kamati ya
Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa
inatarajia kukutana Jumapili (Septemba 2 mwaka huu) kupitia usajili wa
wachezaji kwa msimu wa 2012/2013.
Usajili
utakaopitiwa ni wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Lidi Daraja la Kwanza
(FDL) ambapo Kamati itapitia pingamizi zilizowasilishwa na klabu mbalimbali
dhidi ya wachezaji waliosajiliwa na klabu zingine.
No comments:
Post a Comment