Paul Ince akiwa na mwanawe Thom Ince katika sherehe ya kuzaliwa Thom(Birthiday Bash) |
Blackpool imethibitisha kumuajiri Paul Ince kuwa meneja wa timu yao kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Klabu hiyo inayoshiriki ligi ndogo ya Championship imethibitisha hilo jana jumatatu baada ya bosi huyo wa zamani wa vilabu vya MK Dons, Blackburn na Notts County kumvutia mwenyekiti wa klabu hiyo Karl Oyston
ambaye amesema kuwa Ince ndiye mtu anayestahili kuchukua nafasi ya mtangulizi wake Michael Appleton.
Baba huyo wa mshambuliaji wa Blackpool Tom Ince, ambaye pia ni kiungo nyota wa zamani wa vilabu vya Manchester United, Liverpool na timu ya taifa ya England amekubali kuchukua nafasi ya kocha msaidizi Steve
Thompson, ambaye alikuwa akishikilia nafasi vizuri katika wiki za hivi karibuni kama akiwa kocha wa pili.
Ince anakwenda kuwa baba na bosi wa Tom Ince kama wanavyoonekana katika picha hapo juu mwaka 1994 anaonekana Paul Ince akicheza na mtoto wake Tom na picha ya chini wanaonekana wakiwa katika hafla ya siku ya kuzaliwa Tom ambapo alikuwa akitimiza miaka 21(birthday bash)
Ifuatayo ni kumbukumbu ya baba na mtoto kukutana katika klabu moja kama meneja na mchezaji.
Brian Clough na Nigel Clough
Nottingham Forest – 1984-93
Sir Alex Ferguson na Darren Ferguson
Manchester United – 1990-94
Kenny Dalglish na Paul Dalglish
Newcastle United – 1997-98
Harry Redknapp na Jamie Redknapp
Southampton – 2005
Johan Cruyff na Jordi Cruyff
Barcelona – 1994-96
Steve Bruce na Alex Bruce
Birmingham – 2005-06
na Hull City – 2012- mpaka sasa
Gordon Strachan na Gavin Strachan
Coventry – 1997-2001.
Nottingham Forest – 1984-93
Sir Alex Ferguson na Darren Ferguson
Manchester United – 1990-94
Kenny Dalglish na Paul Dalglish
Newcastle United – 1997-98
Harry Redknapp na Jamie Redknapp
Southampton – 2005
Johan Cruyff na Jordi Cruyff
Barcelona – 1994-96
Steve Bruce na Alex Bruce
Birmingham – 2005-06
na Hull City – 2012- mpaka sasa
Gordon Strachan na Gavin Strachan
Coventry – 1997-2001.
Akinukuliwa Paul Ince baada ya kuthibitihshwa kuwa meneja wa Balckpool amesema
'Ni jambo kubwa mimi kuwepo hapa'
'Fikiria nimekuwa nikifuatilia na kuangalia timu ikicheza katika kipindi cha miezi 14 iliyopita, ni jambo la ina yake kukalia kiti cha umeneja ukizingatia nilikuwa nikiiangalia kama mpenzi lakini nikimfuatilia mtoto wangu akicheza'
'Ni kama niko mwezini na nimefurahi ni jambo kubwa kurejea katika uwanja wa mazoezi wa timu hii'
'
Tom Ince anaonekana akiwa na umri wa miaka miwili akicheza na baba yake, hivi karibuni amekuwa akihusishwa na kutakiwa na Liverpool.
Kazi ya mwisho ya Ince kama meneja ilikuwa akiifundisha Notts County kabla ya kufukuzwa April 2011.
Ince alikuwa ni mchezaji wa kiwango cha juu wa timu ya taifa ya England, Manchester United, Liverpool na Inter Milan.
Paul alikuwepo uwanjani wiki iliyopita akiaangalia mchezo wa timu ya taifa ya England ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 21 mchezo ambao mtoto wake Tom alifunga goli dhidi ya Sweden katika mchezo walioshinda 4-0.
Kinda huyo wa timu ya taifa ya England U21 Tom Ince anazivutia Liverpool na Reading.
No comments:
Post a Comment