Chelsea imefanikiwa kuwashinda Liverpool katika mbio za kumnasa nyota wa FC Basle ya Uswiz Mohamed Salah kwa mtaji wa pauni milioni £11, hizi zikiwa ni taarifa kutoka nchini Switzerland.
'tunaweka wazi dhamira ya Liverpool ya kumtaka nyota huyo wa kimataifa wa Misri na mazungumzo yalifikia katika hatua nzuri mpaka baadaye Blues wakiwa na mlungula mnene wakimzidi Brendan Rodgers'
Wakati Juan Mata akifunga ndoa na Manchester United, Chelsea wameona ni vema wakasaka mbadala wa mhispania huyo kwa kipimo cha Salah ambaye alivutia sana katika mchezo baina yao wa ligi ya mabingwa msimu akifunga katika michezo yote dhidi timu hizo katika hatua ya makundi.
Inaelezwa kuwa chaguo la Salah lilikuwa ni Liverpool, ambako aliamini angepata michezo zaidi yakucheza kikosi cha kwanza lakini mambo ya fedha yamebadili msimamo ikiwa ni pamoja na ushawishi wa Jose Mourinho ukatengua mpango huo kwa Liverpool.
Akivutia huko Ulaya, pia mshambuliaji huyo ameshaifungia timu yake ya taifa jumla ya mabao 17 katika jumla ya michezo 27 aliyocheza.
No comments:
Post a Comment