Klabu ya Barcelona imeitisha kikao cha dharura huku kukiwa na tahadhari kuwa Sandro
Rosell huenda akajiuzulu kutoka katika bodi ya klabu hiyo.
Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya mahakama kuu ya Hispania kukubali kufungua shauri dhidi ya Rosell juu ya madai ya ubadhirifu wa fedha za uhamisho wa Neymar kutoka klabu ya Santos majira ya kiangazi.
Rosell, ambaye alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Joan Laporta mwaka 2010 baada ya kushinda 'landslide vote', amekanusha ubadhirifu huo kuhusu Neymar, lakini huenda akawekwa ndani katika kipindi cha mwaka mmoja au miaka minane endapo atakutwa na hatia.
Makamu wa Rais wa Barca Josep Maria Bartomeu na Javier Faus walikutana na Rosell nyumbani kwake asubuhi ya leo na wanatarajiwa kukutana tena Rais huyo katika 'extraordinary meeting' baadaye pamoja na naibu Rais Joanjo Castillo, mkurugenzi mkuu Antoni Rossich na mkurugenzi wa mawasiliano Albert Montagut.
Nafasi ya Rosell ya kuongoza inatakiwa kumalizika mpaka 2016 na taarifa zinasema huenda Laporta akarejea kwa mara ya pili kushika nafasi hiyo.

No comments:
Post a Comment