Mario Balotelli ametanabaisha kuwa ameshaanza kupenda maisha yake ya kisoka chini ya Clarence Seedolf akidai kuwa kocha huyo mpya ndani ya AC Milan ni kama alivyokuwa Jose Mourinho.
Mshambuliaji huyo mtata alionekana kama hana raha na maisha ya ndani ya klabu hiyo katika nusu ya kwanza ya msimu wakati Rossoneri ilipokuwa ikisaka matokeo na kuambulia matokeo mabovu kiasi kupelekea kuondolewa katika benchi la ufundi kwa aliyekuwa meneja Massimiliano Allegri baada ya kichapo kisicho vumilika cha mabao 4-3 kutoka kwa Sassuolo.
Baada ya kufunga goli la ushindi kwa njia ya mkwaju wa penati katika mchezo wa kwanza wa ushindi chini ya Seedorf ambapo waliwashinda Verona usiku wa Jumapili, Balotelli amempongeza kwa mduchi huyo.
No comments:
Post a Comment