Mabingwa wa Uturuki Galatasaray wametangaza kumuandalia mkataba mnono mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast Didier Drogba kufuatia ombi la mshambuliaji huyo la kutaka kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo ikiwa ni miezi michache imesalia kabla ya mkataba wake wa sasa wa miezi 18 kumalizika kiangazi mwakani.
Rais wa klabu hiyo Unal Aysal amesema mshambuliaji huyo wa zamnai wa Chelsea striker anataka kusalia ndani ya klabu hiyo na kwamba atakabidhiwa mkataba mpya.
Nahodha huyo wa Tembo wa Ivory Coast alijiunga na klabu hiyo akitokea Uchina katika klabu ya Shanghai Shenhua mwezi Januari baada ya kuiba ubingwa wa China klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya huko Super Lig
title.
No comments:
Post a Comment