Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amemsifu sana mshambuliaji wake Fernando Torres baada
ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uhispania kusaidia kuandika bao moja na kufunga bao la
ushindi wakati mechi ikikaribia kuisha na kuwapa ushindi wa 2-1 dhidi ya
wapinzani wao katika Ligi ya Premia Manchester City Jumapili.
Amenukuliwa Mourinho akisema
"Ako macho sana, ana nguvu, na anajiamini,”
Mourinho amewaambia wanahabari baada ya timu yake kupanda hadi nambari mbili kwenye jedwali la uongozi wa ligi
alama mbili nyuma ya viongozi Arsenal, ambao watakutana nao kwenye
mechi ya raundi ya nne katika Kombe la Capital One (League) mnamo
Jumanne.
Torres amekuwa katika hali nzuri sana siku za hivi majuzi na pia
alifunga mabao mawili katikati ya wiki wakati wa ushindi wa 3-0 dhidi ya
Schalke 04 katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Torres alihangaisha sana City hiyo jana, na alisaidia kuunda bao la kwanza
baada ya kumchenga difenda Gael Clichy upande wa kulia na kisha akampa
krosi Andre Schuerrle ambaye aliutuma mpira nyumbani na kupata bao lake
la wkanza akiwa Chelsea dakika ya 33.
Sergio Aguero alisawazisha kwa kombora zito muda mfupi baada ya
kipindi cha pili kuanza lakini Torres baadaye akafunga bao lake la
kwanza Ligi ya Premia msimu huu kwa njia ya kipekee baada ya kupata
mpira kutoka kwa mkanganyiko kati ya Matija Nastasic na kipa Hart.
Nastasic, aliyekuwa ameangalia goli lake, aliupiga mpira kwa kichwa
mbali na Hart na Mhispania huyo akampiku beki wa kushoto wa City Martin
Demichelis kwenye mbio na akautuma kwenye wavu uliokuwa wazi dakika ya
90.
Mourinho alimsifu Torres kwa kujiletea fahari licha ya kupoteza nafasi wazi ya kufunga kipindi cha kwanza.
"Tangu niwasili hapa siku ya kwanza, yeye (Torres) amefanya kazi kwa
bidii sana,” Mourinho alisema.
“Wakati mwingine alikuwa kwenye benchi,
wakati mwingine hakuteuliwa, wakati mwingine nilimwacha nyumbani, na
kila wakati ilikuwa vile vile – anastahili pongezi.”
Torres mwenye furaha tele aliambia Sky Sports: "Kila mpira lazima uwe
mpira muhimu zaidi kwenye mechi kwa sababu unaweza kuwa ndio
utakaokushindia mechi.”
No comments:
Post a Comment