Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) inaanza raundi ya 12 keshokutwa (Oktoba 31 mwaka
huu kwa mechi kati ya Simba na Kagera Sugar itakayofanyika Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Viingilio
katika mechi hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv kupitia TBC 1
vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A.
Nayo
Yanga itashuka uwanjani Novemba Mosi mwaka huu katika mechi nyingine ya
ligi hiyo dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Novemba
2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union
(Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa
Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na
Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Raundi
hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City
itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sokoine jijini Mbeya.
Mechi
za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7
mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs
Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania
Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.
Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment