Mfungaji wa bao la pili Hamisi Kiiza 'Diego' |
Mabao matatu yaliyofungwa na Mbuyu
Twite, Khamis Kiiza (Diego) Didie Kavumbagu na kuipa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mgambo JKT, yametosha kuishusha Simba
kutoka nafasi ya pili hadi ya nne iliyokuwa inashikilia baada ya
jana kufungwa na Azam FC goli 2-1.
Yanga iliandika bao lake la kwanza kupitia kwa Mbuyu Twite akifunga bao hilo akiwa umbali mrefu kutoka langoni mwa wapinzani baada ya kupokea pasi ya Athumani Iddi.
Bao la pili lilifungwa kwa njia ya penati na Hamisi Kiiza kufuatia Didier Kavumbagu kuangushwa ndani ya eneo la hatari.
Bao la tatu liliwekwa wavuni na Didier Kavumbagu baada ya kupokea mpira kutoka kwa Simon Msuva.
Mbuyu Twite akipongezwa na wachezaji wenzake hii leo |
Yanga imefikisha alama 22 ikijikita katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo na hii ni kufuatia matokeo mengine ya ligi hiyo kutoka huko mkoani Mbeya ambako Vijana watukutu wa Mbaye City hii leo kuwalamba kaka zao wa Tanzania Prisons kwa mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine.
Wachezaji wa Mbaye City wakishangilia. |
Azam FC wanaongoza ligi wakiwa na
Pointi 23 sawa na Mbeya City lakini wakitofautiana kwa magoli ya
kufunga Azam FC wakiwa na magoli mengi ya kufunga.
No comments:
Post a Comment