Hatimaye Rais Barcelona Sandro Rosell ametangaza kujiuzulu kuelekea mkutano wa EGM( Extraordinary General Meeting) ambao unatarajiwa kufanyika usiku huu.
Rosell na Barca kwa pamoja wako katika uchunguzi wa mahakama kuu ya Hispania kutokana na tuhuma matumizi mabaya ya fedha za uhamisho wa Neymar kutoka Santos kiangazi iliyopita.
Makamu wa Rais Josep Maria Bartomeu na Javier Faus walikutana na Rosell nyumbani asubuhi ya leo na anatarajiwa kuungana na Rais wa Barca katika 'extraordinary meeting' baadaye hii leo sambamba na naibu Rais Joanjo Castillo, mkurugenzi mkuu wa klabu Antoni Rossich na mkurugrnzi wa mawasiliano Albert Montagut.
No comments:
Post a Comment