Diego Costa amesema kuwa alichagua kuichezea nchi ya kufikia ya Hispania badala nchi yake ya kuzaliwa ya Brazil
kwakuwa kila alichokifanikisha katika soka la kulipwa kimetoka ndani ya nchi hiyo.
Mshambuliaji huyo wa Atletico Madrid ambaye pia ni mfungaji anaye ongoza katika ligi ya nchi hiyo La Liga msimu huu alisaini barua rasmi hapo jana akitangaza rasmi kuwa yuko tayari kuitumikia Hispania katika kikosi cha kocha Vicente del Bosque, maamuzi ambayo yamekuwa ni mwiba kwa kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari.
Amenukuliwa kupitia mtandao wa www.sefutbol.com akisema
"Yalikuwa ni maamuzi magumu lakini kila nilichofanikiwa katika maisha yangu yametoka ndani ya taifa hili(Hispania),"
"Najihisi mwenye thamani hapa kwa kila ninacho kifanya kila siku na naona watu wanavyonichukulia".
Maamuzi ya Costa yamepelekea Scolari kuondoa jina lake katika kikosin chake ambacho kipo katika maandalizi ya michezo miwili ya kimataifa ya kirafikia dhidi ya Honduras na Chile mwezi ujao.
Amenukuliwa Scolari akisema
"A Brazilian player who refuses to wear the shirt of the Brazilian
national side and take part in the World Cup in his own country must
automatically be uninvited,"
No comments:
Post a Comment