Young Africans kesho itashuka katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini
Dar es salaam kucheza na maafande wa jeshi la kujenga Taifa nchini timu
ya JKT Ruvu kutoka mkoani Pwani ikiwa ni muendelezo wa michezo ya Ligi
Kuu ya Vodacom mzunguko wa 12.
Mara baada ya ushindi wa pili mfululizo wa mabao 3-0 dhidi ya Rhino
Rangers na Mgambo Shooting kikosi cha mholanzi Ernie Brandts kimeendelea
kuimarika na safu ya ulinzi ikicheza michezo miwili pasipo kuruhusu
nyavu zake kutikiswa.
Mpaka sasa Young Africans inashika nafasi ya
tatu ikiwa na ponti 22 pointi 1 nyuma ya timu zinaongoza mbili za Azam
FC na Mbeya City zote zikiwa na pointi 23 zikitofautiana kwa mabao ya
kufunga na kufungwa.
Young Africans inahitaji pointi tatu muhimu
katika mchezo huo wa kesho dhidi ya JKT Ruvu ili iweze kujikita kileleni
na kukalia kiti cha uongozi wa Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 25 ambazo
zitaweza kufikiwa na timu mbili tu za Azam FC na Mbeya City ambazo
zitachezwa mwishoni mwa wiki.
Timu iliingia kambini jana jioni
katika hostel zilizopo makao makuu ya klabu mitaa ya Twiga/Jangwani
kujiandaa na mchezo huo ambao ni muhimu kwa vijana wa Jagwani
kuhakikisha wanaendeleza wimbi la ushindi na kupata pointi tatu muhimu.
Katika
mchezo wa kesho Young Africans itakosa huduma ya wachezaji wake David
Luhende na Nizar Khalfani ambao ni majeruhi huku kiungo Haruna Niyonzima
akiukosa mchezo huo kutokana na kuwa nchini Rwanda alipokwenda
kushugulikia matatizo ya kifamilia.
Wapenzi, washabiki na wanchama
wa Young Africans kesho wanaombwa kujitokeza kwa wingi kuja
kuwashangilia vijana katika mchezo wao dhidi ya JKT Ruvu.
No comments:
Post a Comment