Novemba
2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union
(Uwanja wa Mkwakwani, Tanga) ambapo Magambo watakuwa wakiingia uwanjani wakiwa na alama 5 mkiniani mwa ligi hiyo huku Caostal ikiwa na alama 15.
Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa
Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na
Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Raundi
hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City
itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sokoine jijini Mbeya.
Mechi
za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7
mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs
Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania
Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.
Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment