KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, January 29, 2013

TAMKO LA KUONDOKA BARCA LA VALDES LAMCHANGANYA RAIS SANDRO



 Rais wa Barcelona Sandro Rosell amesema mlango bado uko wazi kwa Victor Valdes endapo mlinda mlango huyo atabadili mawazo yake kuamua kusaini mkataba mpya na klabu yake hiyo.

Mapema mwezi huu Valdes aliiambia klabu hiyo kupitia wakala wake kuwa hafikirii kuomgeza mkataba mwingine na Barca baada ya mkataba wake kumalizika june 2014.

Taarifa za mwendelezo zinasema kuwa Barca imekuwa katika mipango ya kufanya usajili mkubwa wa kuziba pengo lake ambapo wamekuwa wakihusishwa na kuwataka walinda mlango wa Liverpool  Pepe Reina, David De Gea wa Manchester United,Marc-Andre ter Stegen wa Borussia Moenchengladbach, Vicente Guaita wa Valencia na Thibaut Courtois ambaye kwasasa yuko kwa mkopo Atletico Madrid.

Kocha wa Barcelona Tito Vilanova na baadhi ya wachezaji kama Andres Iniesta na Lionel Messi wamekaririwa wakisema wanaheshimu maamuzi ya Valdes lakini wanaamini mlinda mlango huyo huenda pia akaamua kusalia katika klabu hiyo.

Katika mchezo wa jumapili ambapo Barca ilishinda 5-1 dhidi ya Osasuna katika dimba la Camp Nou mashabiki walionekana kumpa tano mlinda mlango huyo na kumkubali zaidi tangu alipotoa tamko lake la kusitisha kuongeza mkataba mwingine baada ya kumaliza mkataba wa sasa.

Valdes alijiunga na Barca akiwa kijana mdogo mwaka 1992 na amekuwa na klabu hiyo wakati wote na hakuwahi kutoa tamko lolote la kutaka kuihama klabu hiyo kabla ya katikati ya mwezi huu kupitia wakala wake ambapo alitoa tamko ambalo limeonekana kupingwa na wengi

No comments:

Post a Comment