Mmiliki wa klabu ya Leeds United Massimo Cellino yuko katika mazungumzo na kigogo cha Formula One Red Bull juu ya uwezekano wa kuuzwa kwa klabu hiyo |
Leeds United iko katika uwezekano wa kuuzwa baada ya kuwepo kwa mazungumzo yaliyopevuka na Red Bull.
Kigogo hicho cha F1 kimeonyesha nia kununua klabu hiyo inayoshiriki ligi ndogo ya England maarufu kama Championship
tangu miezi 18 iliyopita lakini pande hizo mbili zilishindwa kufikia makubaliano kwa bei iliyotajwa kuwa ni pauni milioni £40.
Neil Redfearn aliteuliwa kuwa meneja mpya wa Leeds wiki hii kufuatia kufukuzwa kazi kwa mtangulizi wake Darko Milanic
Red Bull imekuwa katika mafanikio makubwa katika michezo ya magari ya Formula One katika miaka ya hivi karibuni
Kwasasa tayari mazungumzo hayo yamerejea huku mmiliki Massimo Cellino, akizua gumzo kubwa kwa kufukuza mameneja wake wawili katika kipindi cha muda mfupi msimu huu.
Taarifa za hivi karibuni zinasema kuwa kiongozi mkuu wa Red Bull amekuwa katika mji wa Leeds tangu jumatano na anaendelea na mazungumzo na kutwaa klabu hiyo
No comments:
Post a Comment