KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, September 8, 2012

MAREKANI HOVYO BILA BRADLEY NA DONOVAN , YAGONGWA NA WACHEZA REGGAE WA JAMAICA


 

Kukosekana kwa kiungo mahiri Michael Bradley na mshambuliaji Landon Donovan mwenye rikodi ya kihistoria katika soka la Marekani kumepelekea Marekani kupata kipigo cha mabao 2-1 toka kwa  wacheza reggae wa Jamaica.
Habari kutoka katika uwanja wa michezo wa Kingston, Jamaica's Independence Park zimesema baada ya kuulizwa kocha wa timu hiyo ya taifa wa Marekani Jurgen Klinsmann kwamba kukosekana kwa Michael Bradley na Landon Donovan ndiyo sababu ya kupokea kichapo hicho katika mchezo muhimu wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia toka Reggae Boyz yuko tayari kwa lawama hizo.
Klinsmann amefafanua kuwa shutuma zote zinapaswa kuelekezwa kwake na kikosi kwa ujumla kwa kuwa walionyesha mchezo butu usiku wa jana.
"vijana waliokuwa uwanjani wanastahili lawama kwa kile kilichotokea.
Bradley amekuwa katika maumivu ya paja aliyo yapata akiwa mazoezini na timu yake ya AS Roma na tangu mchezo wa kwanza dhidi Catania katika ligi  ya Italia Serie A hajashuka dimbani tena mchezo ambao alitoa pasi za mwisho mbili zilizo pelekea matokeo ya na Catania.
Donovan ni majeruhi wa msuli tangu mchezo wa kimataifa wa mwezi uliopita dhidi ya Mexico uliomalizika kwa ushindi wa bao 1-0 uliopigwa katika dimba la Azteca.
Amekaririwa Tim Howard akisema ,
"tulipata matokeo mazuri dhidi ya Mexico mwezi uliopita tulipokuwa na wachezaji wazoefu na hakuna sababu kwa nini tumepoteza mchezo huu"
"Michael kweli ni mchezaji muhimu kwetu na Landon, kama unavyojua wanafanya mambo ambayo yanakuwa, lakini sidhani kama hiyo ndiyo sababu, kweli si dhani hivyo. Nafiri tulikosa umakini katika maeneo fulani"
Klinsmann amesema katika mchezo huo alikuwa na kikosi cha ushindi katika uwanja ambao jina lake la utani ni ‘The Office’ uwanja ambao katika historia yake Marekani ilipata sare mara nne , na sasa wamepoteza.

No comments:

Post a Comment