KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, April 11, 2014

Rais Kikwete apongeza timu ya watoto

Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ameipongeza Timu ya Watoto wa Mitaani ya nchi hiyo kwa kutwaa Kombe la Dunia huko Rio de Janeiro nchini Brazil.

Taarifa iliyotolewa na ikulu ya Tanzania imesema Rais Kikwete afurahishwa jinsi watoto hao walivyonyakua kombe hilo la dunia.

"Mmetuwakilisha vyema, ninawapongeza sana, pia mmewapa moyo watoto wengine wote wenye vipaji maalum lakini hawakubahatika kuwa na makazi rasmi, hongereni sana" Rais amesema.

Timu hiyo ya watoto wenye umri chini ya miaka 16 ilipangwa kundi la 2 ambapo pia zilikuwapo timu kutoka Nchi za Argentina, Nicaragua,Philippines na Burundi.

Makundi yaliyopangwa yalikuwa matatu.

Tanzania iliingia nusu fainali kwa kuwa mshindi wa pili na pia kumenyana na Marekani na kuichapa mabao 6-1 na baadae kuitoa Burundi kwenye fainali kwa mabao 3-1.
"
Hongereni kwa kujituma na kucheza kwa ustadi". Rais amesema na kuwaasa watoto "ongezeni bidii, nidhamu na mazoezi ya kutosha na hakika mtafanikiwa zaidi na kulibeba jina la Tanzania mbali zaidi ya hapa katika ulimwengu wa soka duniani, kwani hakuna kisichowezekana kama mtazingatia maelekezo, mafunzo, bidii na nidhamu ya yote mnayofanya" Ameongeza Rais Kikwete . 


Wakati huo huo Timu ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania iliyotwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani nchini Brazil baada ya kuifunga Burundi mabao 3-1 kwenye fainali imetambulishwa leo (Aprili 11 mwaka huu) katika Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma.

Baadaye timu hiyo leo itapata chakula cha mchana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda. Saa 10 jioni itatembeza kombe hilo katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Dodoma katika gari za wazi.

Jioni imeandaliwa hafla maalumu ya chakula pamoja na burudani hapo hapo mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara.

No comments:

Post a Comment