KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, April 10, 2014

Kuelekea kombe la dunia: Msahambuliaji wa Costa Rica Joel Campbell akosa stika ya kombe la dunia licha ya kununua stika 100

NI NGUMU kuamini kuwa unanua stika 500 za kombe la dunia ambazo zinapicha za wachezaji watakaoshiriki kombe la dunia na usipate kuona jina lako ilhali na wewe ni miongoni mwa wachezaji watakatao kuwepo katika fainali hizo!

Lakini imekuwa hivyo kwa Joel Campbell ambaye alidhani angebahatika kuona moja ya stika hizo ikiwa na picha yake, lakini kumbe alikuwa akijidanganya.

Nyota huyo mshambuliaji kijana wa Arsenal aliye kwa mkopo katika klabu ya Olympiacos, anatarajiwa kuwa ni miongoni kwa wachezaji wa kikosi cha Costa Rica katika fainali zijazo za kombe la dunia nchini Brazil ataonekana akiwa katika kundi moja na timu ya taifa ya Costa Rica,amewekwa katika stika nambari 296 ambazo ni rasmi za nyota wa kombe la dunia.

Mwenyewe ametupia picha za stika 100 alizonunua ambazo ndani kuna picha tano kwa lengo la kusaka picha yake imewekwa katika stika ipi bila mafanikio, ambapo kwa ujumla kuna stika 500 zilizo chapishwa, na hakukuta picha yake

Kuelekea kombe la dunia, kunatarajiwa wachezaji wakubwa kutoka mataifa 32 ambao watashindana katika fainali ambapo unaweza kununu paketi hizo kwa picha tano ndani yake na ikitakiwa kuwepo stika 640 za wachezaji wote.
 
Campbell ni miongoni mwa wachezaji 17 wa Costa Rica kuwa ndani yake pamoja na Bryan Ruiz ambaye ni mshambuliaji wa Fulham anayechezea soka katika klabu ya PSV Eindhoven kwa mkopo.

Ruiz yeye alifanikiwa kuiona stika ya picha yake na kuitupia katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamiii wa twitter hapo jana Jumatano. 

No comments:

Post a Comment