Mauritania itakuwa mwenyeji wa Mauritius Jumamosi katika mchezo wa kwanza wa mzungo wa wa awali wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika 2015.
Mchezo huo utapigwa katika mji wa Nouakchott ambao utakuwa ukiwakutanisha zinazofuatana katika msimamo wa ubora wa shirikisho la soka duniani FIFA kwa upande wa Afrika.
Mauritius, waliochini ya Mauritania katika nafasi ya 45th watawakosa wachezaji wao wawili muhimu.
Kiungo Kevin Bru ameendelea kushikiliwa na klabu yake ya nchini Bulgaria Levski Sofia ambao wanajiwinda na michezo migumu ya ligi ya nchi hiyo ambapo kiungo mwingine muhimu Fabrice Pithia ameamua kuichezea timu ya kisiwa cha Reunion
Jeanne d'Arc.
"Ilikuwa vigumu sana kumalizia kutaja kikosi lakini tutalishughulikia japokuwa ingependeza kama tungekua nao kikosini wote wawili, lakini tutafanya hivyo bila ya wao", Amesema kocha Akbar
Patel.
Timu zote Mauritania na Mauritius zimedhamiria kufuzu kwa mara ya kwanza katika fainali za mataifa ya Afrika katika historia.
Mchezo mwingine ambao ulikuwa uchezwe wikiendi hii wa mzunguko huo wa awali ulikuwa ni baina ya Eritrea dhidi ya Sudan kusini ambao hautachezwa kufuatia shirikisho la soka la nchi ya Eritrean EFF kuitaarifu shirikisho la soka Afrika CAF kuwa wameamua kujitoa katika kampeni hiyo ya 30 ya mataifa ya Afrika ambayo fainali zake zinatarajiwa kufanyika nchini Morocco mwaka 2015.
Hiyo ina maanisha kuwa sasa Sudan ya kusini imefuzu moja kwa moja kuelekea katika mzunguko unaofuata.
No comments:
Post a Comment