Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amepigwa faini ya pauni £8,000 na kupewa onyo kali baada ya kutolewa nje ya uwanja mwezi uliopita katika mchezo ambao walipokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Aston Villa.
Mourinho alifanya kosa la kuingia ndani uwanja kwenda kuongea na mwamuzi Chris Foy sekunde chache baada ya mwamuzi huyo kumuonyesha kadi nyekundu kiungo wake Ramires.
Mourinho alikanusha alipoitwa kusikiliza shauri lake hilo hiyo jana Jumatano.
"sijui ni kwanini nilitolewa uwanjani, nimeuliza lakini mwamuzi amekataa kuniambia"
Ramires alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumrukia kwa miguu miwili mchezaji wa Villa, Karim El Ahmadi, tukio lililozua tafrani pembezoni mwa uwanja.
Mourinho alidai kuwa alikuwa akijaribu kuongea na Foy kwasababu
Ramires alisukumwa na mshambuliaji wa Villa, Gabriel Agbonlahor, ambaye alibadilishwa.
No comments:
Post a Comment