KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, April 10, 2014

Cristiano Ronaldo hoi kwa majeraha ya msuli, sasa kusalia nje kwa muda usiojulikana

Mshambuliaji wa Real Madrid  Cristiano Ronaldo yuko katika hatihati ya kucheza au kutokucheza mchezo wa Jumatano ijayo wa fainali ya Copa del Rey dhidi ya Barcelona kufuatia kukumbwa na majeraha ya misuli.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 29 alikuwa nje ya kikosi cha Madrid kilichoshuka dimbani dhidi ya Borussia Dotmund katika mchezo wa mkondo wa pili wa robo kutokana na kusumbuliwa na mguu.

Real imethibitisha kuwa mshambuliaji huyo amepatwa na majeraha ya katika msuli mkubwa wa mguu wake wa kushoto maarufu kitaalamu kama ' femoris muscle".
Klabu hiyo kongwe hata hivyo imeshindwa kuthibtisha ni kwa muda gani atakuwa nje ya uwanja.

Msimamo wa ligi ya Hispania (La Liga) ulivyo baada ya michezo ya 32.


Points

Wakatia wakielekea kukutana hiyo Jumatano, Atletico wanaonekana kuwa kwenye rekodi nzuri zaidi ya Real, na wakiwa bado kukutana na Barcelona mara mbili.



1. Atletico Madrid
79
2. Barcelona
78
3. Real Madrid
76
Taarifa nchini Hispania zinadai kuwa huenda akasalia nje ya uwanja wa siku 15, na kwamba ataukosa mchezo wa Jumamosi dhidi ya Almeria, fainali ya Copa del Rey dhidi ya Barcelona na mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Nahodha huyo wa Ureno amefunga jumla ya mabao 52, katika michezo 45 aliyocheza katika klabu na timu ya taifa msimu huu.

Hajaonekana uwanjani tangu alipoumia katika mchezo wa kwanza robo fainali dhidi ya Dortmund, ambao alifunga goli katika ushindi wa mabao 3-0.

Ronaldo hakujumuishwa katika mchezo wa jumamosi iliyopita ambao Real waliwafunga Real Sociedad kwa mabao 4-0 mchezo wa ligi La Liga, ambao walishika nafasi ya uongozi wa ligi ambapo alishindwa pia kucheza katika mchezo wa pili wa klabu bingwa ambao walipoteza mbele ya Dotmund kwa mabao 2-0 Jumanne iliyopita, ambapo licha ya kufungwa Real Madrid walisonga mbele kwenye nusu fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2.

No comments:

Post a Comment