Bingwa wa mchezo wa tenisi kwa
upande wa akina dada duniani Serena Williams amekosoa matamshi
aliyoyataja kuwa ya kibaguzi na kutojali ujinsia yaliotolewa na rais wa
shirikisho la Tenisi nchini Urusi Shamil Tarpischev dhidi yake na
dadaake Venus Williams.
Katika mazungumzo yake Tarpischev aliwaita kina dada hao wawili kama ''kaka wawili'' .
Hata hivyo afisa huyo alipigwa
faini ya pauni 15,500 na kupigwa marufuku ya mwaka moja kwa kutoa
matamshi hayo aliyoyataja kama ya mzaha.
''Nadhani matamshi hayo yamejaa ubaguzi na hayajali'' alisema Wiliiams.
''Sikuyapendelea hata kidogo na nadhani watu wengi pia hawakuyapendelea''.
matamshi
ya Bwana Tarpischev pia yalishtumiwa na shirikisho la mchezo wa Tenisi
duniani WTA pamoja na shikisho la mchezo huo nchini marekani USTA.
Hapa Serena na Venus wakiwa katika muonekana halisi wa akina dada achilia mbali umbile la misuli iliyokakamaa kumchanganya |
Hapa walipokutana wenyewe kwa wenyewe |
Akina dada hao licha ya kutajwa kama akina kaka lakini bado wana maumbile ya kuvutia wanaume |
No comments:
Post a Comment