Meneja wa Manchester United Louis
van Gaal amesema lilikuwa ni jambo la kijinga kuwaambia watu kumweka
kwenye mizani baada ya miezi mitatu tu tangu ajiunge na Manchester
United kama kochja wa klabu hiyo
Tangu achukue usukani kama meneja
wa Manchester United hapo Julai alipigiwa debe sana wengi wakisema
kwamba mbinu zake zitaanza kuleta mafanikio baada ya miezi mitatu tu.
Kufikia
sasa miezi mitatu imeisha tangu ajiunge na Manchester United lakini
timu hiyo bado inashikilia nambari ya sita katika orodha ya timu bora
katika ligi ya kadanda ya Uingereza, huku ikiwa imeshindwa mechi mbili.
Van
Gaal,mwenye umri wa miaka 63, alisema: "Lilikuwa jambo la kijinga
kusema miezi mitatu kwa sababu vyombo vya habari vinaongea tu kuhusu
ahadi hiyo ya miezi mitatu.."
Manchester United imeshinda mechi tatu zenye ushindani mkali tangu Van Gaal kujiunga na klabu hiyo msimu huu.
Endapo watashinda mechi dhidi ya West Brom basi huo utakuwa ushindi wa tatu mtawalia katika ligi hiyo ya uingereza .
Hata hivyo Van Gaal amesema timu yake bado haijafanya vya kutosha.
No comments:
Post a Comment