Mabingwa
watetezi Uhispania wamefuzu kuingia fainali ya Euro 2012, baada ya kuishinda
Ureno magoli 4-2, kupitia mikwaju ya penalti, baada ya muda wa kawaida wa
dakika 90 na dakika 30 za ziaida kumalizika kwa timu hizo mbili kushindwa
kufungana.
Bao la
mwisho la mikwaju ya penalti kwa Uhispania lilitiwa wavuni na Cesc Fabregas, na
kuwapa wenzake matumaini ya kutetea ubingwa wao kikamilifu, watakapocheza aidha
na Ujerumani au Italia katika fainali ya Jumapili.
Fabregas,
ambaye ni kiungo cha kati wa timu ya Barcelona, alipiga mkwaju ambao baada ya
kugonga mwamba upande wa kushoto, ulitambaa wavuni, na ikawa ni tiketi ya
Uhispania kufanya mipango ya kusafiri hadi Kiev, Ukraine, kwa fainali.
Mchezaji wa
Ureno, Bruno Alves, alielekea kuwa na wasiwasi, na kushindwa kufunga mkwaju
wake, baada ya mpira kugonga mwamba, na Ronaldo, akiwa amepangwa na timu yake
katika nafasi ya tano kwa wapigaji penalti, hakupata hata nafasi ya kutimiza
wajibu huo.
Wengine
waliokosa kufunga kupitia mikwaju ya penalti ni mchezaji wa Ureno, Joao
Moutinho, wakati kipa wa Uhispania, Casillas, alipoweza kuokoa kwa kuruka
upande wa kkulia.
Awali
mchezaji wa Uhsipania Xabi Alonso naye alikosa kutumbukiza wavuni mkwaju wa
penalti, licha ya kwamba ulikuwa ni mkwaju wa kasi na uliopigwa kwa nguvu,
lakini kipa Rui Patricio akauzuia.
No comments:
Post a Comment