Mshambuliaji
wa Mario Gomez amesema kwake yeye kusugua benchi sio tatizo, fahari yake ni kuona Bayern Munich inatwaa
taji la Bundesliga mwisho wa msimu.
Mshambuliaji
huyo amekuwa akisugua benchi baada ya kupata majeraha tangu siku za mwanzo za
kuanza msimu msimu wa 2012-13 lakini amesisistiza hilo si tatizo kikubwa ni
kutwaa taji kuliko kurejea katika kikosi cha kwanza.
Amenukuliwa na
gazeti la Bild akisema
"ki
ukweli lengo langu kubwa ni kushinda taji la Bundesliga. Mambo mengine si
muhimu kuliko taji".
Gomez ameshinda
mataji mawili mpaka sasa akianza kupata taji msimu wa 2006-07 akiwa na Stuttgart
na baadaye akiwa na Bayern msimu wa 2009-10.
Pazzini: AC Milan inabidi ikaze buti
Giampaolo
Pazzini amesisitiza kuwa AC Milan inabidi kuongeza uwezo wake wa kiuchezaji
katika wiki za hivi karibuni ili kupunguzo kupoteza michezo kama ilivyokuwa
katika miezi ya mapema ya kuanza ligi msimu huu wa 2012-13.
Milani
imekuwa ikifanya vizuri katika mfulilizo wake wa michezo saba ya ligi kuu ya
Italia ‘Serie A’ katika siku za hivi karibuni, lakini Pazzini ameonya hiyo
isiwe kigezo cha kubweteka na matokeo hayo katika sehemu iliyosalia ya msimu
Amenukuliwa na
Sky Sport Italia akisema
"tulianza
vibaya na morali ilikuwa chini na matokeo hayakuwa mazuri"
Milan watarejea
katika mfululizo wa michezo ya Serie A nyumbani dhidi ya Pescara jumapili.
No comments:
Post a Comment