KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, December 12, 2012

Drogba sasa kuvaa uzi wa Juventus kwa mkopo na Zambia yadai Messi amepora rekodi ya Godfrey Chitalu kupeleka vielelezo fifa.



Mshambuliaji Shanghai Shenhua na timu ya taifa ya Ivory coast Didier Drogba ameingia mkataba na bibi kizee cha Turin, Juventus kuitumia mwezi January.

Drogba mwenye umri wa miaka 34 ambaye ameendelea kufanya mazoezi na klabu yake ya zamani ya Chelsea kwa lengo la kujiweka fiti, alishindwa kupata uhamisho kabla ya mwezi Januari, baada ya ombi lake kukataliwa na shirikisho la soka duniani fifa kufuatia kubanwa na sheria za uhamisho wa kimataifa za shirikisho hilo.

Hata hivyo mshambuliaji huyo amefanikiwa kupata uhamisho huo ambao kimsingi una lengo la kutaka kulinda na kuimarisha kiwango chake kabla ya fainali za mataifa ya Afrika zitakazo fanyika nchini Afrika kusini wakati huu ambapo msimu wa ligi ya nchini China ukiwa umemalizika.

Fainali za mataifa ya Afrika zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi January 19.

Juventus ambao ni mabingwa wa taji la nchini Italia wamekuwa wakimtaka Dagba kwa kumpatia mkataba wa muda mrefu wa mwaka mmoja na nusu mpaka kumalizika kwa msimu wa 2013-14 lakini Drogba akitaka mkataba wa muda mrefu zaidi mpaka June 2015.

Juve ilikuwa ikisaka mshambuliaji mwingine mpya na ilikuwa ikihusishwa na kuwataka Luis Suarez na Edin Dzeko.



Zambia yapinga rekodi ya messi fifa
Marehemu Godfrey Chitalu enzi zake.
Kikosi cha Zambia timu ya taifa ya Zambia kilichopata huduma ya Chitalu.

Chama cha soka cha Zambia ZFA kimepinga rekodi iliyowazi ya mshambuliaji Lionel Messi ya ufungaji wa mabao mengi zaidi katika kipindi cha mwaka mmoja.

Messi alitengeneza rekodi hiyo katika mchezo wa ligi kuu ya nchini Hispania ‘Primera Division’, baada ya kufunga magoli mawili dhidi ya Real Betis mchezo uliochezwsa jumapili iliyopita na kufikisha jumla ya mabao 86 na kuipita rekodi ya mjerumani Gerd Muller ya mabao 85.

Chama cha soka cha Zambia FA kimedai kuwa wana ushahidi ambao watauwasilisha kwa shirikisho la soka duniani FIFA ambayo inaonyesha kuwa mshambuliaji wa Kabwe Warriors ya nchini humo Godfrey Chitalu alifunga mabao 107 mwaka huo 1972 ambao Muller aliweka rekodi hiyo.

Msemaji wa ZFA ameliambia gazeti la Soccer Laduna kuwa

"sisi tuna rekodi hiyo, ambayo ilirokodiwa na chama cha soka cha Zambian, lakini haikuweza kurikodiwa na FIFA"

Amesema wakati dunia ikimtangaza Lionel Messi kuvunja rekodi ya Gerd Müller gumzo liliibuka hapa kwanini dunia haitambui magoli ya Godfrey.

Chitalu, ambaye alishinda tuzo ya mchezaji bora wa Zambia alifunga magoli katika mashindani matano tofauti ya ndani akiwa na klabnu yake pia akiwa na timu ya taifa.

No comments:

Post a Comment