KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, November 16, 2013

Arsenal yamuongezea mkataba Wojciech Szczesny

Mlinda mlango wa Arsenal Wojciech Szczesny amesaini mkataba mpya na klabu yake hiyo ambao umeelezewa kuwa ni wa muda mrefu"long-term contract".
Mlinda mlango huyo wa kimataifa wa Poland alijiunga na vinara hao wa Premier League akitokea katika klabu ya nyumbani kwao Poland ya Legia Warsaw mwaka 2006 na kuanza kuitumikia kwa mara ya kwanza klabu hiyo Septemba 2009.
Ukilimlinganisha na mwenzake Pole Lukasz Fabianski, mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 23 ameshaichezea Gunners jumla ya michezo 123.
Wojciech Szczesny ni mtoto wa mlinda mlango wa zamani wa kimataifa wa Poland Maciej Szczesny, ambaye aliwahi kutolewa nje ya uwanja kwa kumuumiza Roberto Mancini usoni.

"Ilikuwa ni michuano ya Ulaya (European Cup Winners) mchezo wa robo fainali mwaka 1991," Szczesny ameliambia gazeti la Guardian mwezi Februari 2011.

"Ukitafuta katika ukurasa wa YouTube utathibitisha hilo. Ni pigo la wazi. Alikwenda moja kwa moja kumfanyia hivyo" 

Arsenal haijaweka bayana urefu kwa mkataba huo mpya na Szczesny, ambaye amesema klabu hiyo ni kama familia yake "like my family".
Szczesny, ambaye alikuwa na mkataba wake wa mwisho aliingia mwaka 2010 amesema
"Najivunia kuwa mchezaji wa Arsenal na naangalia ya mbele kuisaidia klabu yetu kwenye mafanikio miaka ijayo." 

Baada ya kung'ara na Arsenal msimu huu pia alipata nafasi ya kuichezea Poland katika mchezo dhidi ya England ambao kwake ulikuwa ni mchezo wa kimataifa wa 15 na ulikuwa ni mchezo wa kusaka tikiti ya kufuzu kombe la dunia mwezi Oktoba katika dimba la Wembley. 

Meneja wa GunnersArsene Wenger amesema 
"Nimefurahi sana, siku zote nimekuwa nikiamini kuwa ni mchezaji mwenye kipaji mwenye ubora na akili"

No comments:

Post a Comment