Kiungo wa Real Madrid Sami Khedira atakuwa nje ya uwanja kwa miezi sita kufuatia kupata maumivu ya mguu.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 ametonesha mguu wake wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya timu ya timu yake ya taifa ya Ujerumani dhidi ya Italia katika mchezo uliopigwa usiku wa jana ambao ulimalizika kwa sare ya 1-1.
Khedira, ambaye alikuwa akikamilisha mchezo wa 44 wa kuitumikia Ujerumani sasa atalazimika kufanyiwa upasuaji wa msuli.
"Hii ni mbaya kwa Sami," amenukuliwa meneja wa Ujerumani Joachim Low.
"Amekuwa siku vizuri na ndio maana nadhyani kuwa atakuwa sawa wakati michuano ya fainali za kombe la dunia itakapokuwa ikianza."
Wasufu wa Sami Khedira
Kuzaliwa: April 4 1987, mjini StuttgartSehemu ya uchezaji : Kiungo
Vilabu alivyochezea: Stuttgart (2006-2010), Real Madrid (2010-mpaka sasa)
Mataji: German Bundesliga (2006-07), Spanish Copa del Rey (2010-11), Spanish La Liga (2011-12).
Kimataifa: Michezo 44.
Khedira amekuatana na maumivu hayo wakati wa kipindi cha pili wakati akikabiliana na kiungo wa Italia Andrea Pirlo.
Ujerumani ni miongoni mwa mataifa ambayo yanapewa nafasi kubwa ya kushinda taji la dunia nchini Brazil baada ya kufuzu kwa kushinda michezo yake tisa ya kuwania kufuzu kati ya michezo kumi waliyocheza.
Kikosi cha Low kinaendelea na maandalizi yake ya kombe la dunia kwa kucheza michezo ya kimataifa ya kiarafiki na Jumanne itakuwa na mchezo mwingine dhidi ya England katika dimba la Wembley.
Khedira alianza kucheza soka katika klabu yak Stuttgart na baadaye kuelekea Bernabeu kwa ada ya uhamisho isiyokuwa wazi kwa mkataba wa miaka mitano mwezi Julai 2010 baada ya kungara katika fainali ya kombe la dunia nchini Afrika kusini mwaka 2010.
No comments:
Post a Comment