KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, October 4, 2013

MOURINHO: SIJUTII KUMTOA LUKAKU KWENDA EVERTON

Kocha wa kikosi cha Chelsea Jose Mourinho amesisitiza kuwa hajutii kumtoa Romelu Lukaku kwa mkopo akidai kuwa kucheza Everton ni kitu kimoja na kucheza Chelsea".
Kwasasa mreno huyo anao washambuliaji Samuel Eto'o, Demba Ba na Fernando Torres katika orodha ya washambuliaji wake.

Lukaku, kwasasa amekuwa katika kiwango cha kuvutia akirejea katika kasi ya ufungaji wa mabao yake 17 wakati huo katika kikosi cha West Brom ambapo sasa ana mabao matatu katika michezo miwli aliyoicheza Everton huku Roberto Martinez akisema kuwa Chelsea haiwezi kumuita tena mshambuliaji huyo.

 Alipoulizwa endapo anajutia kumtoa mshambuliaji huyo, Mourinho amewaambia wana habari kuwa,
 
"No. It is one thing to play for Everton and another to play for Chelsea."

Sare ya bao 1-1 Jumamosi dhidi ya Tottenham imeiacha Chelsea katika ushindi wa mchezo mmoja katika michezo minne iliyocheza na kujiweka katika alama nne nyuma ya vinara wa ligi hiyo Arsenal.

Mourinho anadhani klabu hiyo, kama ilivyo kwa Manchester United, walikuwa katika ratiba ngumu ya kuanza msimu na ameomba uvumilivu ya kuanza kuchomza na ushindi.
 

No comments:

Post a Comment