Paul Were na Kevin Omondi. |
Kocha James Nandwi. |
KOCHA wa
timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars James Nandwa amewatimua wachezaji wake
wawili tegemeo katika kikosi chake kufuatia kutoroka kambi ya timu yao hapo
jana usiku.
Wachezaji hao
ni winga Paul Were na kiungo Kevin Omondi ambapo wachezaji hao waliondoka na
kuelekea kwenye starehe baada ya kupewa pesa zao za posho au Bonas ya mchezo
wao dhidi ya Sudani Kusini ambao walichomoza na ushindi wa mabao 2-0.
Taarifa zinasema
wachezaji hao walitoweka katika kambi yao iliyoko katika hoteli ya Sky Sports iliyoko
Kireka na kwenda kustarehe usiku mzima wakichanganywa na posho walizopewa
kufuatia ushindi.
Mbaya zaidi
wachezaji hao walirejea hotelini na machangudoa jambo ambalo kocha James Nandwa
amekielezea kitendo hicho kuwa ni cha aibu na kisichokubalika.
Kevin Omondi
alikuwa katika kiwango kizuri katika mchezo wao dhidi ya Sudani Kusini hapo
jana ambapo alitoa pasi za mwisho zilizo zaa magoli yote mawili ya Harambe ukiwa
ni ushindi wa kwanza kwa Harambee Stars.
Wachezaji hao
wanatarajiwa kurejea Nairobi huku adhabu zaidi zikiwasubiri kutoka shirikisho
la soka la Kenya (FKF) alivyo nukuliwa Francis Nyamweya.
No comments:
Post a Comment