KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, November 28, 2012

KILIMANJARO STARS WASUBIRISHWA KUFUZU NA BURUNDI. SUDANI YAWANYOA WASOMALI

Selemani Ndikumana nahodha wa Burundi akishangilia goli la penati dhidi ya Kilimanjaro Stars.
Timu ya taifa ya Burundi( Intamba murugamba) imeungana na timu ya taifa ya Uganda ‘Uganda Cranes’ kutinga hatua ya robo fainali ya Cecafa Tusker challenge Cup 2012 baada ya kuichapa Tanzani Bara maarufu kama Kilimanjaro stars kwa bao 1-0 mchezo ulifanyika katika uwanja wa Mandela maarufu kama Namboole jioni ya leo.

Sulemani Ndikumana ambaye ndiye nahodha wa Burungi alifunga goli hilo kwa njia ya penati kunako dakika ya 50  mchezo baada ya kufanyiwa madhambi na mlinzi Shomari Kapombe katika eneo la hatari.

Kikosi cha kocha Kim Poulsen kilianza kwa uzuri mchezo huo huku Mrisho Ngassa, Mwinyi Kazimoto na Simon Msuva wakifanya mashambulizi kwa kupiga mashoti langoni mwa lango Burundi ambapo mlinda mlango wa Burundi Burundi Arthur Arakaza akijitahidi kuzuia michomo yao.

Kwa upande wa Burundi washambuliaji Selemani Ndikumana na Amissi Tambwe hawakuwa nyuma kulisakama lango la Kilimanajaro Stara lakini mlinzi Shomari Kapombe alikuwa imara kuongoza ulinzi katika eneo lake la hatari.
Farid Muhammad akipongezwa na wenzake baada ya kufunga goli la Sudan.
Katika mchezo wa mapema bao la dakika za mwisho la Farid Muhammad  liliweza kuisaidia timu ya taifa ya Sudani kuweza kuizamisha Somalia waliokuwa wagumu hii leo mchezo pia uliofanyika katika dimba la Namboole mapema mchana.

Mshambuliaji huyo alifanikiwa kuvunja mtego wa kuotea uliwekwa na washambuliaji wa Somalia kunako dakika ya 87 mpira ambao ulimpa tabu mlinda mlango wa Somalia Abd Elrahman Ali kuweza kuudaka.

No comments:

Post a Comment