Frank
Lampard ameweka wazi kuwa siku za utumishi wake katika klabu ya Chelsea sasa
zinahesabika wakati huu ambapo maekuwa ni sehemu ya wachezaji wa kocha wa muda Rafa
Benitez.
Kiungo huyo
mwenye umri wa miaka 34 ambaye amekuwa mtumishi katika klabu hiyo kwa zaidi ya
miaka 10, alikuwa na matumaini ya kumaliza kabisa uchezaji wake wa soka katika
klabu hiyo ambayo amefanikiwa kutwaa mataji 3 ya ligi kuu ‘Premier League’,
mataji manne ya kombe la FA na msimu uliopita akifanikiwa kushinda taji kubwa
la vilabu barani ulaya ‘UEFA Champions League’.
Amenukuliwa na
Telegraph akisema,
"nadhani
nina miaka miwili au mitatu ambayo nitaendelea kuwepo katika kiwangu cha juu, Pengine
mambo hayawezi kudumu milele”
Akiwa amefunga
mabao karibu 200 akiwa na Chelsea Lampard anajivunia kuwepo Stamford Bridge katika
kipindi chote akiwa hapo na ana amini kuna mengi ambayo ameyafanya ikiwa hata
kutwaa taji la vilabu ulaya.
Juan Jesus anasema Inter lazima achukue Scudetto.
Mlinzi wa Inter
Milan Juan Jesus amesema kuwa kikosi kima cha timu yao kinaamini kuwa wanauwezo
wa kutwaa taji la ligi kuu ya nchini Italia ‘Scudetto’, namkuweka wazi kuwa
kila mmoja amejidhatiti kuhakikisha Juventus inaondoka katika uongozi wa ligi Serie
A.
Wakiwa nyuma
kwa alama nne, bado mlinzi huyo wa kimataifa wa Brazil anaamini kuwa wachezaji
wenzake watafanya kila linalo wezekana kutwaa taji hilo ambalo wanalisaka tangu
mwaka 2010.
Akiongea na
Sport Mediaset amekaririwa akisema,
"siku
zote tunaamini kuwa tunaweza kushinda Scudetto, na ninataka kufanya kila kitu
kinachowezekana kulinyakua taji hilo"
"Inter ni klabu kubwa tutafanya kila
linalo wezekana kushinda"
Pia mlinzi
huyo amezungumzia jinsi alivyo fanikiwa kuyazoea maisha ya nchini Italia na
sasa anaeleza wazi kutamani kuendelea kuishi San Siro kwa muda mrefu.
"ninafurahia
kwasababu kulikuwa hakuna mtu aliyekuwa ananijua hapa Italia lakini sasa mambo
yamebadilika. Ninatamani kuwa na miaka mingine zaidi mitano au sita kuonyesha
uwezo wangu. Nataka kuwa sehemu ya Inter kwa muda mrefu.
Shinji
Kagawa arejea mazoezini .Nimanja Vidic kunguruma dhidi ya Sunderland kesho.
Meneja wa
mashetani wekundu Manchester United Sir Alex Ferguson amethibitisha kuwa kiungo
wake has confirmed that midfielder Shinji Kagawa atarejea katika mazoezi yake
kama kawaida wiki ijayo kwa kuwa hivi sasa anaendelea vizuri.
Kiungo huyo
aliyesajiliwa msimu wa uhamisho wa kiangazi akitokea Borussia Dortmund amekuwa
nje ya uwanja tangu Oktoba wakati United ilipocheza dhidi ya Braga mchezo wa
vilabu bingwa Ulaya ambapo Kagawa alipatwa na maumivu ya mguu.
Pia kuna
taarifa njema kwa mashabiki wa United ambapo Nemanja Vidic nikiwa kuimarisha
afya yake na anatarajiwa kuwepo dimbani jumamosi katika mchezo dhidi ya Sunderland
utakaopigwa Old Trafford.
Mzee Furgauson
amenukuliwa akisema
"Nemanja
anarejea kikosini kesho , lakini Jonny Evans ni wazi kuwa atakuwa nje baada ya
maumivu ya wiki iliyopita.
No comments:
Post a Comment