Mshambuliaji wa Toto African Pastol Makula akijaribu kuwatoka mabeki wa Mtibwa kwenye mchezo wa mashindano ya uhai uliochezwa leo asubuhi uwanja wa Karume, |
Mshambuliaji wa Toto wa African Heri Mohamed akijaribu kumtoka beki wa Mtibwa Mrindwa Mathias kwenye mchezo wa mashindano ya uhai leo asubuhi uwanja wa Karume, Mtibwa ilishinda bao 3-1. |
Mtibwa
Sugar ya Morogoro leo asubuhi (Desemba 14 mwaka huu) imeibuka na
ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Toto Africans ya Mwanza katika mechi ya
michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za vijana wenye umri
chini ya miaka 20 (U20) za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom.
Juma
Luzio alifunga mabao yote matatu (hat trick) katika mechi hiyo
iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.
Alifunga mabao hayo dakika za 44,81 na 88.
Hata
hivyo, Toto Africans ndiyo walioanza kufunga katika mechi hiyo ya kundi
A. Bao hilo katika michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Said
Salim Bakhresa kupitia maji Uhai lilifungwa dakjika ya 22 na Pastol
Makula.
Nayo
Simba imenguruma baada ya kuitandika Mgambo Shooting ya Tanga katika
mechi nyingine ya michuano hiyo iliyochezwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa
Azam ulioko Chamazi. Wafungaji kwa washindi walikuwa Ramadhan Mdoe
dakika ya 19, Mohamed Salum dakika ya 77 na Ramadhan Singano dakika ya
89.
Michuano
hiyo inaendelea leo mchana na jioni. Mechi ya Ruvu Shooting na Kagera
Sugar iliyokuwa ichezwe mchana Uwanja wa Azam, Chamazi sasa itafanyika
saa 10 kamili jioni katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Mechi
nyingine za leo ni Coastal Union vs JKT Ruvu (mchana- Karume), African
Lyon vs Azam (jioni- Chamazi). Vilevile mechi kati ya JKT Oljoro na
Yanga inachezwa leo Uwanja wa Chamazi.
Kesho
(Desemba 15 mwaka huu) ni mapumziko, na michuano hiyo itaendelea
Jumapili kwenye viwanja vyote viwili- Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na
Uwanja wa Azam- Chamazi.
No comments:
Post a Comment