CAF KUFANYA UKAGUZI WA ‘LESENI ZA KLABU’ JANUARI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) litatuma ofisa wake nchini mwezi ujao
kwa ajili ya kufanya ukaguzi kwenye klabu za Ligi Kuu ya Tanzania kabla
ya kutoa leseni kwa zile ambazo zitakuwa zimekidhi vigezo vilivyowekwa.
Ili klabu ishiriki mashindano ya CAF ni lazima iwe na leseni hiyo.
Kwa
mujibu wa CAF, ofisa huyo atakuwa nchini kuanzia Januari 7 mwakani
ambapo atafanya ukaguzi huo hadi Januari 14 mwakani. Mbali ya ukaguzi
katika klabu, pia ofisa huyo atakagua viwanja vitakavyotumika katika
mashindano yake na hoteli ambazo timu kutoka nje zitakuwa zinafikia
kabla ya mechi.
Baadhi
ya masharti kabla ya klabu kupewa leseni ya CAF ni pamoja na kuwa na
ofisi (physical address), uwanja wake wa mazoezi, programu ya maendeleo
kwa vijana, sekretarieti ya kuajiriwa, hesabu za fedha zilizokaguliwa
(audited accounts) na benchi la ufundi linaloundwa na watu wenye sifa
zinazostahili.
No comments:
Post a Comment