KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zantel imejitokeza kudhamini Mkutano
Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Waandishi
wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utakaofanyika Desemba 21 na 22 mwaka huu Kiromo View Resort Hotel, Bagamoyo mkoani
Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es
Salaam jana, Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Zantel Ahmed Seif Mohamed, alisema
wanajisikia furaha kushirikiana na TASWA kudhamini mkutano huo wa aina yake.
Alisema Zantel imekuwa na uhusiano mzuri na
wanahabari, hivyo walipoombwa hawakusita kufanya hivyo na wana matumaini
makubwa utakuwa mkutano wenye manufaa.
Alieleza kuwa kampuni yake baada ya kupata
mafanikio katika mashindano ya Epiq Bongo Star Search iliyomalizika hivi
karibuni ni nafasi nyingine ya kuendelea kudhamini matukio mbalimbali ya
michezo na burudani kwa kadri uwezo utakavyoruhusu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa TASWA, Juma
Pinto aliishukuru Zantel na kusema awali chama hicho kiliomba udhamini kwa
kampuni hiyo kwa lengo la kufanya mkutano Dar es Salaam, lakini sasa walifikiria
ufanyike Bagamoyo, Pwani.
Alisema Zantel wamedhamini kwa kiasi cha Sh
6,040,000 na kwamba bajeti ya mkutano huo ni Sh milioni 20, hivyo kuomba wadau
wengine wasaidie ili kufanikisha mkutano huo utakaohusisha zaidi ya waandishi
wa habari za michezo 100 ambao ni wanachama wa TASWA.
“Mkutano huo unatarajiwa kushirikisha
wanachama 100, na pia watakuwepo wadau mbalimbali wa TASWA wakiwemo waandishi
wakongwe wa habari za michezo wambao watapewa nafasi ya kuzungumza kwenye
mkutano huo,” alisema Pinto.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa chama hicho,
aliwasisitiza wanachama kuendelea kuthibitisha ushiriki wao na kuwa mwisho wa
kufanya hivyo ni kesho alasiri.
No comments:
Post a Comment