Coastal
Union ya Tanga imeendelea kufanya vizuri kwenye michuano ya kuwania
Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa
klabu za Ligi Kuu ya Vodacom baada ya jana (Desemba 12 mwaka huu)
kuifunga Toto Africans mabao 3-1.
Mabao
ya Coastal katika mechi hiyo ya kundi A iliyochezwa Uwanja wa Chamazi
yalifungwa na Mohamed Miraji dakika ya 44, Abdul Banda (dk. ya 62) na
Ramadhan Shame (dk. ya 83). Toto Africans ndiyo iliyoanza kupata bao
dakika ya 30 lililofungwa na Severin Constantine.
Coastal
Union ilishinda mechi yake ya kwanza mabao 2-1 dhidi ya Tanzania
Prisons katika michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Said Salim
Bakhresa kupitia maji Uhai.
Nayo
Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya African Lyon katika
mechi ya kundi B iliyochezwa leo asubuhi (Desemba 12 mwaka huu) Uwanja
wa Karume. Miraji Athuman na Ramadhan Mzee ndiyo walioifungia Simba
dakika ya 15 na 47 wakati la African Lyon lilifungwa dakika ya 57 na
Mbela Kashakala.
Polisi
Morogoro iliifunga Azam bao 1-0 kwenye Uwanja wa Karume wakati katika
Uwanja wa Azam, JKT Ruvu iliifunga Tanzania Prisons bao 1-0 lililofungwa
dakika ya 16 na Jacob Mambia. Yanga na Ruvu Shooting zilitoka suluhu
kwenye Uwanja wa Chamazi.
Katika
mechi iliyochezwa leo asubuhi (Desemba 13 mwaka huu) Uwanja wa Karume,
Oljoro JKT imeizamisha Kagera Sugar mabao 3-0. Mabao hayo yamefungwa na
Hamis Saleh dakika ya 49 huku Shamir Mohamed akipachika mawili dakika ya
52 na 55.
Michuano
hiyo itaendelea kesho (Desemba 14 mwaka huu) kwa michezo kati ya Mtibwa
Sugar vs Toto Africans (asubuhi- Karume), Coastal Union vs JKT Ruvu
(mchana- Karume), Oljoro JKT vs Yanga (asubuhi- Chamazi), Ruvu Shooting
vs Kagera Sugar (mchana- Chamazi), Mgambo Shooting vs Simba (asubuhi-
Chamazi) na African Lyon vs Azam (jioni- Chamazi).
No comments:
Post a Comment