Serikali
kupitia Bodi ya Taifa ya Utalii, imeendesha semina ya washiriki wa Fainali za
Taifa Miss Utalii Tanzania 2012/13 iliyo fanyika leo Katika ukumbi wa mikutano
uliopo Makao makuu ya Bodi ya utalii Tanzania.
Semina
hiyo ambayo ilifunguliwa na Kaimu mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania
ambaye pia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi hiyo Ndugu Devotha Mdachi,
imeandaliwa na Bodi ya Utalii kwa lengo la Kuwapiga msasa washiriki hao kabla ya
fainali ya Taifa itakayo fanyika 17.03.2013 katika ukumbi wa Dar
Live.
Akifungua
Semina hiyo Ndugu Devotha mdachi pamoja na kuwakaribisha washiriki wote makao
makuu ya Bodi ya Utalii Tanzania aliwaasa washiriki hao kujifunza na kuvielewa
kwa kina vivutio vya utalii Tanzania ili wale watakao shinda na kupata nafasi ya
kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia waweze kuitangaza vema Utalii
wa Tanzania na nchi kwa Ujumla.
Aliwakumbusha pia wao kama warembo wa utalii
wanalo jukumu la kuunda mkono juhudi za Serikali kuhamasisha utalii wa Ndani
lakini pia jukumu la kutangaza vivutio vya utalii wa Tanzania kimataifa na
Kimataifa.
Aliendelea kuwaasa pia wao kama warembo wa utalii wanapaswa kujivunia
utanzania na Maliasili zake huku wakidumisha Mila na Utamaduni wa Tanzania na
kwamba siku zote wanatakiwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu na mfano wa kuigwa
katika jamii kwa maana warembo wa utalii ni alama ya Urithi wa Taifa na
kielelezo cha Mwanamke wa Kitanzania.
Aliwakumbusha wale watakao shinda kwenda
kutetea Mataji ya Dunia ambayo Miss Utalii Tanzania wanashikiria .
Nae
mtoa mada Mkuu katika semina hiyo Ndugu Deogratias Malogo ambaye ni Meneja wa
Utafiti na Maendeleo wa Bodi ya Utalii Tanzania aliwafahimisha warembo wa Miss
Utalii Tanzania wa Fainali za Taifa 2012/13 kuwa secta ya utalii ni secta muhimu
katika Uchumi na kuchangia pato la Taifa kila mwaka. Alisema Secta ya utalii
inachangia zaidi ya asilimia 20 ya pato la tTaifa kila mwaka na zaidi ya
asilimia 25 ya pato la taifa la fedha za kigeni kila Mwaka.
Alisema Kidunia
secta ya utalii inachangia zaidi ya asilimia 12 ya ajira zote
Duniani.
Warembo
hao walifundishwa Historia ya utalii Tanzania . Walifundishwa vivutio vya utalii
Tanzania, Mbinu za kutangaza utalii wa Tanzania Kitaifa na Kimataifa, lakini
aliwaelezea pia jitihada ambazo serikali kupitia bodi ya taifa ya utalii na
Mamlaka nyengine za utalii nchini imekuwa ikifanya katika kukuza secta ya utalii
na kutangaza vivutio vya utalii kitaifa na Kimataifa.
Ndugu Malogo aliwaelezea
juu ya umuhimu wa utalii wa ndani katika kukuza na kuchangia pato la utalii la
Taifa na kwamba wao kama warembo wa utalii ni sehemu muhimu katika kukuza na
kuendeleza secta ya Utalii Tanzania kwani wao ni kioo cha jamii na mfano wa
kuigwa kitabia Mwenendo Muonekano na Hulka.
Aliwatakia kila laheri wale watakao
shinda katika fainali hizo za Taifa kwenda kuwa mabarozi bora wa Tanzania katika
mashindano ya Dunia watakayo kwenda Kushiriki.
Nae
Rais wa Miss Utalii Tanzania alitoa shukurani na Pongezi kwa Bodi ya Utalii
Tanzania kwa juhudi kubwa wanazo fanya ya kuinua na kuendeleza secta ya utalii
nchini.
Alipongeza na kushukuru pia hatua ya bodi ya utalii, kwa kuendesha
Semina Maalum kwa washiriki wa fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania 2012/13
na kusema kwamba semina hii itakuwa ni Dira na ufunguo kwa Miss Utalii Tanzania
wa kutwaa mataji zaidi ya Dunia katika mashindano yote watakayo shiriki na pia
katika kutangaza na kuhamasisha utalii wa ndani Kitaifa na
Kimataifa.
No comments:
Post a Comment