Meneja wa klabu ya Celtic, Neil
Lennon amesema itakuwa ni vugumu kwa klabu hiyo kuwabakisha wachezaji wake
waliovutia katika michuano ya klabu bingwa Ulaya.
Licha ya kufanikiwa kutinga hatua ya
kumi na sita bora ya michuano hiyo mikubwa ya vilabu barani Ulaya, bado vinara
hao wa ligi kuu ya soka nchini Scotland(SPL) wameshindwa kusonga mbele katika
hatua ya robo fainali baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa
Juventus mchezo uliochezwa mjini Turin na hivyo kuondoshwa kwa ushindwa wa jumla
wa mabao 5-0.
Lennon amesema itakuwa vigumu
kuendelea kuwa na wachezaji ambao wanataka kuendeleza vipaji vyao licha ya
kwamba sera ya klabu hiyo ni kuchukua vipaji , kuviendeleza na kuwauza.
Jumla ya wachezaji watatu wa wa
kikosi cha Lennon wanatarajia kumaliza mikataba yao hivi karibuni wakati ambapo
mshambuliaji Gary Hooper na mlinzi Victor Wanyama mikataba yao ikitarajiwa
kumalizika majira ya kiangazi mwaka 2014 na tayari wamekataa kuongeza mikataba ndani ya
klabu hiyo yenye msakani yake katika jiji la Glasgow.
Kwa upande wake kiungo Joe Ledley,
ambaye anatarajiwa kuwa huru baada ya msimu huu, bado hajafungua mazungumzo
mapya juu ya hatma yake ya baadaye.
Baada ya kuloweshwa katika uwanja wa
nyumbani kwa kichapwa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa mjini
Glasgow, Celtic ilijikuta katika wakati mgumu na kupoteza matumaini ya kutinga
hatua ya robo fainali ambapo jana mabao ya Alessandro Matri na Fabio
Quagliarella yakazima rasmi ndoto za klabu hiyo.
Hata hivyo Lennon amewapongeza
wachezaji wake kwa kufikia hatua hiyo ya michuano.
No comments:
Post a Comment