Venue: Luzhniki Stadium
Date: 7 March 2013
Kick-off: 17:00 GMT
Mshambuliaji
wa Newcastle Papiss Cisse atakuwa nje ya uwanja usiku wa leo katika mchezo wa kwanza
wa hatua ya 16 bora wa ligi ndogo ya UEFA (Europa League last 16) dhidi ya Anzhi Makhachkala.
Cisse hakusafiri
kuelekea nchini Russia kutokana na kusumbuliwa na misuli, hivyo kufanya uwezekano wa
nafasi yake kuchukuliwa na Shola Ameobi.
Meneja Alen Pardew amelazimika kumjumuisha mlinzi Fabricio
Coloccini pamoja na winga Hatem Ben Arfa ambao anatarajia
kuwatumia usiku wa leo.
Ben Arfa hajaonekana
dimbani tangu alipopatwa na maumivu ya msuli mwezi desemba katika mchezo ambao
timu hiyo ilifungwa na Fulham kwa mabao 2-1 mchezo wa ligi kuu ya soka nchini
England.
Kikosi cha Pardew kitakuwa na kazi kubwa kukabiliana na wakali kama mshambuliaji wa
zamani wa Barcelona Samuel Eto'o na kiungo wa zamani wa Real Madrid Lassana
Diarra.
Mlinda
mlango namba moja ambaye kwasasa nia majeruhi wa enka Tim Krul amesalia jijini Newcastle, ambapo Alan Pardew
amelazimika kuwachukua walinda mlango makinda Jak Alnwick na Adam Campbell katika
safari hiyo.
Kwa upande
wa meneja wa Anzhi, Guus Hiddink anadhani kikosi chake kitacheza bila presha
kwakuwa kimefanikiwa kufikia malengo waliyojiwekea wakati wa maandalizi ya msimu ambayo ni kufikia hatua ya 16.
Amenukuliwa akisema
"Kwakweli
tunafuraha sana kwa kufikia dhamira yetu tuliyojiwekea tangu mwanzo wa msimu
ambayo ni kuendelea kuwepo mpaka kipindi cha majira ya baridi katika michuano
ya Ulaya
BERNITEZ KUMKOSA DEMBA BA DHIDI YA STEAUA BUCHAREST.
Venue: National Arena, Bucharest
Date: Thursday 7 March
Kick-off: 18:00 GMT
Bosi wa muda
wa Chelsea Rafael Benitez atakuwa na kazi kubwa ya kukumbana na timu ya
ushindani ya Steaua Bucharest katika michezo ya michuano ya Ulaya hatua ya 16
bora ukiwa ni mchezo wa mkondo wa kwanza utakao pigwa usiku wa leo National
Arena katika jiji la Bucharest.
Chelsea wako katika mawindo ya kucheza mchezo wa
robo fainali wa michuano ya FA ambao utapigwa jumapili wakati huohuo wakiwa
katika kampeni kubwa ya kumaliza katika moja ya nafasi nne za katika ligi kuu
ya soka nchini England.
Benitez usiku
wa leo anatarajiwa kufanyia mabadiliko kikosi chake lakini pia anaonekana
ni mwenye matumaini makubwa ya kusonga mbele katika michuano hiyo ya Ulaya.
Steaua
Bucharest imepoteza michezo mitano tu katika jumla ya michezo 20 ya michuano ya
Ulaya iliyocheza ikiwa katika dimba lake la nyumbani wakati ambapo Chelsea imemudu
kushinda michezo 4 tu katika jumla ya michezo 12 iliyocheza ikiwa ugenini
katika michezo ya Ulaya.
Demba Ba amekosa
uhalali wa kucheza katika mchezo huo utakao pigwa nchini Romania kutokana na
kwamba amekwisha kuchezea Newcastle katika michuano hii mwanzoni mwa msimu,
wakati ambapo Victor Moses yeye hajasafiri na kikosi hicho hivyo kumfanya Bernitez
kulazimika kumtumia Fernando Torres katika kikosi cha kwanza.
Chelsea ilishindwa
kuendelea kutetea taji lake la ubingwa wa Ulaya baada ya kutolewa katika mzunguko
wa kwanza wa michuano hiyo mwezi desemba.
Mlinzi David
Luiz anasema yeye na wachezaji wengine wa kikosi cha Chelsea wana njaa na
mafanikio ya Ulaya wakati huu ambapo
Steaua wakimkosa
mshambuliaji wao muhimu Stefan Nikolik ambaye ana matatizo ya mguu.
No comments:
Post a Comment