SERIKALI
yazidi kulikaba koo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kuwataka
kuitisha mkutano mkuu wa marekebisho ya katiba kabla ya Aprili 15 huku
wakitakiwa kufanya uchaguzi kabla ya Mei 25 mwaka huu.
Habari zinasema kuwa Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara amekataa kupangiwa siku ya kuonana na viongozi wa TFF na badala yake aliwataka jana kufika ofisini kwake kwa ajili ya kikao walichoomba. Hata hivyo Waziri alitarajiwa kusafiri jana usiku kwa muda wa siku 10.
Juzi TFF kupitia kwa Katibu mkuu wake Angetile Osiah alisema wamewasilisha barua kwa Waziri Mukangara kutaka kukutana naye Alhamisi (kesho) na kama ikishindikana wakutane baada ya March 13 na kwamba wanamtaka Naibu Waziri Amos Makala akae kando katika suala lao kwa vile ameshaonyesha ana upande anaoupendelea.
Lakini hata hivyo katika barua iliyokwenda Wizarani ambayo ilisaniwa na katibu huyo wa TFF yenye Kumb:Na: TFF/ADM/MIYCS.13/03 ya March 4 imeomba kukutana na Waziri bila ya kuweka angalizo la kumtaka Naibu Waziri Amos Makalla kukaa kando tofauti na alivyotangazia vyombo vya habari.
Katika kikao cha jana kilichofanyika ofisini kwa Waziri mbali na Waziri Fenela mwenyewe pia alikuwepo naibu wake Amos Makala na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi na katibu wake Henry Lihaya wakati kwa upande wa TFF walioudhuriwa ni Angetile Osiah, Mkurugenzi wa ufundi Sunday Kayuni na mwanasheria wa TFF ambaye aliwakilisha kamati ya utendaji Alex Mgongolwa.
"Mchakato wa uchaguzi unaanza upya, wameambiwa waitishe mkutano mkuu wa marekebisho ya katiba na kuingiza marekebisho yote kuanzia ya mwaka 2007 hadi 2010 kwa kuwa katiba iliyopo kwa Waziri ni ile ya mwaka 2006 na wamepewa siku 40 toka sasa watekeleze ilo la mkutano wa marekebisho ya katiba kabla ya Aprili 15 yawe yameshafanyika.
"Pia wamepewa siku 40 nyingine kwa iyo jumla ni siku 80 baada ya marekebisho ya katiba uanzie mchakato wa uchaguzi na hadi Mei 25 uchaguzi mkuu uwe umeshafanyika na pia TFF wametakiwa ndani ya siku tano kuanzia leo (jana) hadi Marchi 11 Jumatatu kuhakikisha wameshatoa msimamo wa kutekeleza agizo la Serikali.
Chanzo hicho kimesema kuwa katika mkutano wa marekebisho ya katiba pia maazimio yatapitishwa kwa njia ya kupiga kura za uwazi kwa kunyoosha mkono ndio au hapana na pia kufuatia agizo hilo la Serikali kamati ya rufaa chini ya Idd Mtiginjola itakuwa imekufa kibudu huku ile ya Profesa Mgongo Fimbo ndio itakayopewa jukumu la kuendelea na zoezi la Kamati ya rufaa.
Akizungumzia suala hilo Katibu mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema "Nimewaoneni mmeingia Wizarani, wambieni wawape taarifa huko mimi siwezi kuzungumza chochote sijapata barua yoyote kutoka Wizarani."
Hata hivyo kwa upande wa Wizara walisema kuwa tayari wameshawapelekea TFF barua na kwamba TFF ndio yenye jukumu la kutangaza yale yaliyozungumzwa kwenye kikao chao na Waziri.

michuzi.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment