KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, June 19, 2012

Robbie Keane:Trapattoni atasalia



Kocha wa timu ya taifa ya Ireland Giovanni Trapattoni hatalazimishwa kuondoka licha ya kikosi cha timu ya taifa ya Ireland kuonyesha kiwango kibovu hii ikiwa ni kauli ya nahodha Robbie Keane.
Matumaini yalikuwa ni makubwa wakati Trapattoni akiingoza timu ya taifa katika hatua za mwisho za michuano mikubwa kwa mra ya kwanza ndani ya kipindi cha miaka kumi lakini kipigo katika mchezo wa ufunguzi cha mabao 3-1 dhidi ya Croatia, na kufuatia kichapo kingine cha mabao 4-0 toka kwa Hispania na kupoteza mchezo mbele ya Italia kwa mabao 2-0 kimeifanya timu hiyo kurejea nyumbani bila hata point moja.

Ulinzi mbovu kukosekana kwa mipango katika sehemu ya ushambuliaji kumezua maswali mengo endapo kuna haja ya kuendelea kupata huduma ya ufundishaji toka kwa kocha huyo mwenye umri wa miaka 73 katika zijazo.
Lakini Trap anasema anataka kusalia Keane alipoulizwa kuhusu kama kuna uwezekano wa kuondoshwa kocha amesema “No chance.”
 Kiungo Keith Andrews aliondoshwa dimbani katika mchezo dhidi ya Italia alipoulizwa alionekana kumtetea Trapattoni akisema
"tuwe wakweli hatujafuzu fainali hizi kwa karibu miaka  24 ni rahisi kukaa chini na kumkosoa mtu aliyetufikisha katika hatua ya kufuzu . Hatuwezi kubadili kitu ambacho kimetuletea mafanikio kwa zaidi ya miaka minne?

No comments:

Post a Comment