KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, June 19, 2012

Contento saini mkataba mpya Bayern Munich mpaka 2016


Mlinzi wa kushoto Diego Contento ameamua kuongeza kuda wa kuendelea kutoa huduma ya uchezaji soka katika klabu yake ya Bayern Munich inayoshiriki ligi kuu ya kandanda chini Ujerumani maarufu kama Bundesliga na sasa ataendelea kuwepo katika klabu hiyo kwa mika mingine minee
Bayern Munich imetangaza hilo kupitia mtandao wa klabu kuwa Diego Contento ameongeza mkataba kwa Bavarians mpaka June 2016.
Mkataba wake wa waali ulikuwa umalizike majira ya kingazi mwakani 2013 na tayari klabu mbalimbali kubwa barani ulaya vilashaanza kumnyemelea.

Kwa hatua hiyo mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 22-amemaliza sasa tetesi juu ya hatma yake baada ya kusaini kuendelea kusalia kwa miaka mingine mitatu.
Contento ni zao la Bayern youth wenyewe kwani alianzia katika kituo cha vijana wadogo kabla ya kunza kuingia katika soka la wakubwa mwaka 2010. Nyota huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 ameshaitumikia klabu hiyo jumla ya michezo 47.

No comments:

Post a Comment